AFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA NA TRENI AKIIDANDIA MALAMPAKA SIMIYU


Kamanda wa Polisi, mkoa wa Simiyu, ACP Richard Abwao.

Na Sitta Tumma - Simiyu
Mtu mmoja, Galula Luhende, mkazi wa Malampaka, Wilaya ya Maswa, Mkoa wa Simiyu, amefariki dunia baada ya kugongwa na Treni.

Mtu huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 45 na 50, miguu yake yote miwili pia ilikatwa na Treni baada ya kumkanyaga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Richard Abwao, amethibitisha akisema ajali hiyo imetokea jana, saa 3:00 usiku.

Kamanda Abwao amesema Treni hiyo ilikuwa ikitokea jijini Mwanza kwenda Dar es Salaam, kwamba kabla ya ajali ilisimama Malampaka kupakia abiria.

"Marehemu alikuwa akidandia Treni hiyo iliyokuwa imeanza kuondoka, ndipo alipoteleza na kuanguka na kukanyagwa miguu.

"Marehemu huyo kabla ya kufariki dunia, alikimbizwa Kituo cha Afya Malampaka na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Maswa kwa matibabu," ACP Abwao amenukuriwa.


Kulingana na tukio Hilo, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa raia kuwa na tahadhari ya kiusalama, punde wawapo eneo la Stesheni ya Treni.


Kamanda Abwao ametoa rai hiyo pia kwa wananchi wakati wanapokuwa karibu na njia ya Gari Moshi (Treni).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post