MBUNGE WA ZAMANI MOSHI VIJIJINI DR. CYRILI CHAMI AFARIKI DUNIA


Aliyewahi kuwa mbunge wa Moshi Vijijini, Dr. Cyrili Chami, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Novemba 5, 2020, katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma, alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Chami alihudumu kama mbunge wa Moshi Vijijini kuanzia mwaka 2005, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akiwa Mbunge, Rais wa Awamu ya nne, Mh Jakaya Kikwete, alimeteua Januari 4, 2006, kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje.

Alihuduma katika Wizara hiyo ya Mambo ya Nje kabla ya Februari 12, 2008, kuhamishwa na kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara  kabla ya kuwa Waziri kamili wa Wizara hiyo kuanzia mwaka 2010 hadi 2012.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post