JOB NDUGAI ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA USPIKA WA BUNGE | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, November 3, 2020

JOB NDUGAI ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA USPIKA WA BUNGE

  Malunde       Tuesday, November 3, 2020Spika wa Bunge anayemaliza muda wake, Job Ndugai amechukua fomu kwa ajili ya kutetea nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.

Ndugai ambaye amekuwa katika nafasi hiyo katika Bunge la kumi na moja amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo na kuirejesha leo katika ofisi makao makuu ya CCM jijini hapa.

Akizungumza baada ya kurejesha fomu kwa Katibu msaidizi idara ya oganaizesheni CCM Taifa, Solomon Itunda, Ndugai amewaomba Watanzania wamuombee ili chama kimteue katika nafasi hiyo.

"Ni utaratibu wa chama chetu wa kidemokrasia kuruhusu wanachama wenye sifa kugombea nafasi ya Spika na Naibu Spika kisha kufanya uteuzi. Niwaombe Watanzania waniombee ili niteuliwe na niwaambie kuwa wakati ukifika tutaongea nao," amesema Ndugai.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post