BUNGE LAMCHAGUA DK. TULIA ACKSON KUWA NAIBU SPIKA


Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamemchagua Mhe.Dkt. Tulia Ackson kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa Naibu Spika wa Bunge la 12.

Dkt. Tulia ameshinda kwa kishindo baada ya kupata  kura 350 ambapo  wapiga kura walikuwa 354 .

Uchaguzi huo umefanyika leo tarehe 12 Novemba 2020, jijini Dodoma ambao ulitanguliwa na uthibitisho wa jina la Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

Akiomba kura kwa wabunge Mhe. Dkt. Ackson amesema kuwa atajitahidi kuwatumikia wabunge wote bila kujali tofauti za kisiasa ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha amesema kuwa atamshauri  vizuri Spika juu ya Sheria na Kanuni kwa kutumia uzoefu alionao  ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wote.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post