RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI..YUMO RAIS MSTAAFU WA ZANZIBAR NA MWAKYEMBE


Kushoto ni Dkt. Harrison Mwakyembe na kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Rais Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamesd Shein, kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, akichukua nafasi ya Jaji Mstaafu, Barnabas Samatta, ambaye amemaliza muda wake.

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Novemba 24, 2020, kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, ambapo pia Rais Magufuli, amemteua Dkt. Harrison Mwakyembe, aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), akichukua nafasi ya Mariam Joy Mwaffisi.

Mwingine aliyeteuliwa hii leo ni aliyewahi kuwa Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka, ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), akichukua wadhifa huo kwa kipindi cha pili sasa.

Uteuzi wa viongozi wote hao watatu unaanza hii leo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post