HATIMAYE TRUMP AKUBALI KUANZA KUMKABIDHI OFISI JOE BIDEN | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, November 24, 2020

HATIMAYE TRUMP AKUBALI KUANZA KUMKABIDHI OFISI JOE BIDEN

  Malunde       Tuesday, November 24, 2020

Rais mteule Joe Biden Kushoto na rais Trump kulia

Donald Trump amekubali kuanza kwa mchakato rasmi wa kumkabidhi madaraka Rais mteule Joe Biden.

Rais amelitaka shirika linaloshughulikia mabadilishano hayo "lifanye kile kinachostahili kufanywa", hata wakati anaahidi kuendelea kupinga matokeo.

Ofisi ya utawala wa huduma za serikali imesema inamtambua Bwana Biden kama "mshindi".

Hilo linawadia wakati Bwana Biden ameidhinishwa rasmi kama mshindi wa jimbo la Michigan na kuwa pigo kubwa kwa Trump.

Timu ya Bwana Biden imefurahishwa na kuanza kwa mchakato huo wakati rais mteule anajiandaa katika sherehe za kuapishwa Januari 20,2021.

"Uamuzi wa leo ni hatua iliyohitajika kuanza kukabiliana na changamoto zinazokumba taifa letu ikiwemo kudhibiti ugonjwa wa virusi vya corona na kuboresha uchumi tena," taarifa iliyotolewa imesema.

"Uamuzi huo ni hatua ya kiutawala ya kuanza rasmi kwa mchakato wa mabadilishano ya madaraka na mashirika husika."

Mapema Jumatatu, Bwana Biden alizindua timu itakayoangazia sera ya fedha na usalama wa taifa iliyojumuisha watu wa zamani wa miaka hiyo katika utawala wa Obama.

Biden atamchagua Anthony Blinken kuwa waziri wa mambo ya nje na John Kerry kama mjumbe wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, huku Janet Yellen ikidokezwa kwamba ndiye atakayekuwa mwanamke wa kwanza kuwa waziri wa fedha.

Trump aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter wakati ofisi ya utawala wa huduma za serikali ambayo ndiyo yenye jukumu rasmi la kuanza mchakato wa mabadilishano ya madaraka inaarifu timu ya Biden kwamba itaanza mchakato huo.

Afisa wa ofisi hiyo Emily Murphy alisema dola milioni 6.3 sawa na (£4.7m) amezitenga kwa ajili ya rais mteule.

Wakati anaahidi kuendelea na "vita hivyo muhimu", rais alisema: "Haidhuru, kwa maslahi ya nchi yetu, Napendekeza Emily na timu yake kufaya kile kinachostahili kwa kuzingatia itifaki za awali na pia nimearifu timu yangu kufanya vivyo hivyo."
Chanzo - BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post