TIGO YATOA ZAWADI ZA SIMU JANJA ZAIDI YA 200 KWA WASHINDI WA KAMPENI YA NCHI NZIMA YA ‘JAZA TUKUJAZE TENA’


Dar esalaam, Ijumaa, 13 Novemba 2020 – Kampuni inayoongoza katika kuhakikisha mtanzania anaishi maisha ya kidijitali, Tigo Tanzania, leo imetoa zaidi ya simu janja 167 kwa washindi wa kila siku na wiki wa kampeni ya ‘Jaza Tukujaze Tena’ inayoendelea nchi nzima. Kampeni hiyo ambayo ilizinduliwa tarehe 23 Oktoba mwaka huu, itafanyika kwa kipindi cha miezi mitatu huku ikiwapa fursa wateja wa Tigo kuweza kujishindia zaidi ya simu janja 1200 pamoja na ofa za papo kwa papo kila wanaponununua vifurushi vya muda wa maongezi, SMs pamoja na data. Simu janja zinazoshindaniwa ni pamoja na Samsung Note 20, ITEL T20 na Smart Kitochi.
Simu zote hizi zinasubiri washindi ambao ni wateja wote wa Tigo, wauzaji wa jumla wa bidhaa za Tigo, Mawakala, Viongozi wa timu za mauzo, na watoa huduma wakubwa wa huduma za Tigo pesa. Akizungumza wakati wa kukabidhi simu janja kwa washindi, Meneja Huduma kwa wateja Kanda ya Pwani, Beatrice Kinabo, amesema, “Tangu tuzindue kampeni hii, tumetoa zawadi ya dakika za muda wa maongezi zaidi ya milioni 231, MB za data milioni 815 na SMS milioni 109 kwa wateja wetu nchi nzima ambao walinunua vifurushi tangu kuzinduliwa kwa kampeni hii. Leo hii tunakabidhi simu janja kwa washindi wa kila siku na wiki”. Ili wateja waweze kupokea ofa za papo hapo, wanapaswa kununua aina yoyote ya kifurushi, kiwe cha siku, wiki au mwezi kupitia njia zote za manunuzi zinazotambuliwa na Tigo ikiwa ni pamoja na kupitia menu kuu ambayo ni *147*00#, Tigo Pesa App na Tovuti. Baada ya manunuzi, wateja wataingizwa moja kwa moja kwenye droo ambayo itakuwa inawaweka kwenye nafasi nzuri ya kujishindia simu janja. 
Wauzaji wa jumla wataingizwa kwenye droo hii moja kwa moja na watakuwa na nafasi ya kuibuka washindi wa simu janja endapo watauza aina yoyote ya kifurushi cha Tigo kupitia Tigo Rusha. Tigo Tanzania inapenda kuwataadharisha wateja wake wote kwamba wawe makini na matapeli wanaoweza kuibuka kupitia mgongo wa kampeni hii. Wateja wanapaswa kufahamu kwamba, zawadi zote za bando zitakuwa zinatolewa papo hapo mara tu baada ya mteja kununua bando. Pia washindi wa simu janja wa kila siku pamoja na wiki watapigiwa simu na mfanyakazi wa Tigo kupitia namba maalumu ya kampuni mara tu baada ya droo hizo kufanyika. Ofa hii ni bure, washindi hawapaswi kutoa malipo ya aina yoyote ili kupata zawadi zao. Wateja wote wa Tigo wanashiriki katika ofa hii na washindi wa simu janja watapigiwa simu kupitia namba 0713800800.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post