SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LIMETOA HUDUMA KWA NCHI 192

Posta Masta Mkuu Wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang'ombe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 146 ya Posta duniani na kuweka wazi mikakati ya Shirika hilo kujikita katika mfumo wa kidijitali ili kuongeza faida.
Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Hassan Mwang'ombe akizungumza na wateja waliofika kupata huduma katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 146 ya Posta duniani. Shirika hilo linatoa huduma ya usafirishaji mizigo kwa nchi 192.
Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang'ombe akimsikiliza moja ya mteja aliyefika kupata huduma katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 146 ya Posta duniani. Shirika hilo linatoa huduma ya usafirishaji mizigo kwa nchi 192.
Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang'ombe akielezea ukarabati utakaoendana na mfumo wa Kidijitali unaofanywa katika ofisi za Posta Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 146 ya Posta duniani. Shirika hilo linatoa huduma ya usafirishaji mizigo kwa nchi 192.
Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang'ombe akiangali utendaji kazi wa wafanyakazi wa Shirika la Posta Ofisi za Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 146 ya Posta duniani. Shirika hilo linatoa huduma ya usafirishaji mizigo kwa nchi 192.

*WAADHIMISHO YA MIAKA 146 YA POSTA

 

Na MwandishiWetu,Dar es Salaam

Katika kuadhimisha miaka 146 ya Posta duniani, Shirika la Posta limewaasa Watanzania kutumia huduma ya Posta kwa ajili ya maendeleo ya nchi ikiwemo kutoa huduma ndani na nchi 192 duniani.

Shirika Posta nchini limefanya maadhimisho hayo na kuweka wazi mikakati yake ya kutumia teknolojia ya kisasa ili kuongeza ufanisi kwenye kazi zao na kuwahudumia watanzania wote.

Akizungumza na waandishi wa Habari Dar Es Salaam, katika maadhimisho ya miaka 146 ya posta duniani, Posta Masta Mkuu wa shirika hilo,Hassan Mwan'gombe Shirika limeweza kupata faida kubwa na kuweza kutoa gawio la serikalini Milioni 350 kutokana na mfumo wa kidijitali.

Mwang'ombe amesema mfumo wa Kidijitali umeweza kuwasaidia na. kuboresha shughuli za shirika hilo ndani na nje ya nchi na kujiinua kiuchumi na kupata faida kubwa.

Amesema, Shirika linafanya huduma ya kusafirisha mizigo nchi 192 ambazo zinapata huduma hiyo na limeweza kuhakikisha mizigo ya wateja inafika kwa usalama mkubwa na uaminifu.

Aidha, Mwang'onde ameeleza Shirika la Posta lipo mbioni kuzindua huduma ya Posta mkononi kama njia ya kuwarahisishia wateja wao kupata huduma popote waliopo.

"Wateja watajisajili kwa njia ya simu na kwa sasa hivi mteja hatajihitaji kufuata barua yake katika sakundu la Posta bali itamfuata alipo."

Amesema, Posta ni zaidi ya barua kwani wanasafirisha bidhaa mbalimbali wana magari yanayosafirisha vitu nchi nzima na pia wana mpango wa kuwa na boti yao ili kurahisisha usafiri wa mizigo.

Akielezea kwa kina kuhusiana na huduma ya Posta wakati wa mlipuko wa virusi vya Corona, Mwa'gombe amesema "katika kipindi cha maambukizi ya virusi vya COVID 19 serikali ilitupatia jukumu la kusafirisha sampuli kutoka eneo moja hadi na tulifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa sana."

Nakuongeza kuwa Shirika hilo lilikuwa miongoni mwa kudhibiti janga hilo.

Pia baada ya mkutano huo kulifanyika ziara fupi ya kutembelea baadhi ya vitengo vinavyotoa huduma ya kusafirisha na kupokea mizingo ya wateja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments