Serikali Yazindua Kichwa Kimoja Cha Treni Ambacho Ni Miongoni Mwa Vichwa Saba Vilivyozinduliwa Na Kugharimu Tsh.bilioni13


 Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
SERIKALI ya awamu ya Tano chini ya uongozi wa Raisi Dk. John Magufuli imeendelea kutimiza yale ambayo ilidhamiria kuyakamilisha kama ahadi kutoka katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kuboresha miundombinu katika sekta mbalimbali hapa nchini.

Katika kufanikisha hayo Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imefanya maboresho ya kimiundombinu kupitia Shirila la Reli Tanzania TRC  kwa kukarabati kichwa cha Garimoshi kati ya Vichwa saba ambavyo vimedhamiliwa kufanyiwa maboresho na Shirika hilo la Reli.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Kichwa hicho  cha Garimoshi [Treni]katika Ofisi za TRC Kanda ya Kati Dodoma  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi . Isaack Kamwelwe alisema Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa JPM imejipanga kupitia Wizara husikaya Kusaidia Shirika la Reli TRC katika ufanisi na kukabiliana na Changamoto za uendeshaji zinazowapata Shirika hususani katika usafirishaji  wa kusogeza Mizigo kwa kupunguza gharama za uendeshaji.

Pia, Mhandisi Isaack Kamwelwe na hapa alielezea  faida ya ukarabati wa vichwa hivyo vya treni ikiwa ni Pamoja na kuwa na usafiri wa uhakika,kuongeza kasi mwendo kutoka kilometa 35 kwa saa hadi kilometa 70 kwa sa

Aidha alisema Ukarabati wa kichwa hicho kimoja kilicho karabatiwa kati ya saba ambavyo vinatarajiwa kukarabatiwa umefanywa na nguvu za Watanzania kutokana na malipo ya kodi pamoja na kushirikiana na Kampuni inayotoka Nchini Maleysia katika karakana iliyokuwa Morogoro.

pia alisema ubora wa kichwa  hicho kitakuwa na uwezo wa kusogeza mabehewa ya  kusukuma mizigo katika maeneo mbalimbali ya vituo vya Garimoshi hapa Nchini Ili kuboresha huduma ya usafirishaji katika Shirika  la Reli Tanzania, aidha Kamwelwe alisema kichwa hicho kitakuwa na uwezo mkubwa wa kusukuma mabehewa ya mizigo zaidi ya ishirini kutokana na uwezo wake kufikia hourse power 4000 Mpaka 8000 na kitakuwa na uwezo wa kutumia mafuta ya diesel pamoja na umeme.

katika kufanikisha ukarabati wa vichwa hivyo saba vya Garimoshi Serikali ilitenga Fedha za Kitanzania Bilioni kumi na tano (15)  kufanya maboresho ambapo kichwa kimoja kimeghalimu fedha Bilioni 1.5 hivyo vitakuwa na uwezo mkubwa kutokana na ukarabati walioufanya kupitia kampuni ya nje ya nchi yenye wafanyakazi wazawa kutoka Tanzania wenye weredi na ufanisi mzuri wa kukarabati.

"Nimefurahi sana kuona Serikali ya JPM inavyoendelea kufanya maboresho katika sekta mbalimbali, leo hii tunafanya uzinduzi wa kichwa hiki cha Garimoshi ambacho kimekarabatiwa na wastaafu wa Shirika la Reli ambao wanafanya kazi katika kampuni Kutoka Nchini Malaysia" alisema Kamwelwe.

Katika uboreshaji huo wa Miundombinu ya TRC Serikali imejenga reli ya Kisasa Ambayo vipande vya Dar es Salaam,Morogoro Mpaka Makutupola, Singida  vinaendelea kujengwa na reli hiyo ya kisasa yenye kilometter 722 imeghalimu fedha za Kitanzania Trilion  7.1 ikiwa ni fedha halali za kodi wanazolipa  Watanzani na tayari Wizara imekwisha tia saini ya makubaliano ya ununuzi wa vichwa Tatu  na mabehewa 44 ambavyo vitaendeshwa kwa umeme na vitakuwa na hourse power 3000.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments