NITAHAKIKISHA FEDHA ZA TASAF ZINAWANUFAISHA WALENGWA-UMMY MWALIMU

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akizungumza wakati wa mkutano wake wa kampeni  kata ya Msambweni Jijini Tanga
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kulia akimnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Msambweni (CCM) Godias Kimati
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akizungumza wakati wa mkutano wake wa kampeni  kata ya Msambweni Jijini Tanga
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akifurahia jambo wakati akiwa meza kuu kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba na kushoto mgombea Udiwani wa Kata ya Msambweni (CCM) Godias Kimati
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kulia akicheza sambamba na msanii wa bongofleva Shilole wakati wa mkutano huo wa kampeni
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kushoto akisalimiana na msaani wa mziki wa Bongofleva nchini Shilole kabla ya kuimba wakati wa mkutano wake wa kampeni
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akipandisha bendera ikiwa ni ishara ya kufungua shina la wakareketwa kwenye kata ya Msambweni
Umati mkubwa wa wananchi wa Kata ya Msambweni wakimsikiliza Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu
Umati mkubwa wa wananchi wa Kata ya Msambweni wakimsikiliza Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu
Umati mkubwa wa wananchi wa Kata ya Msambweni wakimsikiliza Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu
Wasanii wa mziki wa Bongofleva nchini Kassim Mganga kulia akiwa na Shilole wakifuatilia kwa umakini mkutano wa mgombea ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema kwamba endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo atahakikisha fedha za Tasaf zinawanufaisha walengo na si wengine kama ilivyo sasa.

 

Uummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Msambweni katika mkutano wa kampeni wa kuomba wampe ridhaa.

Alisema kwamba katika Kata ya Msambweni anafahamu kero mojawapo inayowasumbua wao na wana Tanga ni ni fedha za Tasaf kutowafikia walengwa na hali hii inasabishwa na baadhi ya watendaji wetu wasio waaminifu ambao huwapatia fedha watu wasiostahili kupewa.

“ Niwaambie jambo hili nimeanza kulifanyia kazi tutahakikisha wakazi wa Msambweni na Tanga nzima wanaostahili  kupata fedha za Tasaf  wanapata”Amesema Ummy Mwalimu.

Aidha pia Ummy ameahidi kutatua changamoto ya Elimu kwakusukuma maboresho ya Miundombinu katika Shule ya Msingi Msambweni na Sekondari yake ili kuondosha kero zilizopo.

“Lakini pia sijalisahau Daraja kutoka Chuo cha Zaharau hadi Ofisi ya Kata na kusafisha dimbwi la Maji linalozalisha mbu katika Mtaa wa Msambweni C “Alisema

Hata hivyo alisema kwamba atakikisha pia anaifanyia kazi changamoto ya kata hiyo kutokuwa na Zahanati hatua inayowalazimu kwenda kwenye kata nyengine kupata huduma hiyo.

 

“Kata hii ya Msambweni haina zahanati niaminini jambo hilo nitalifanyia kazi kuhakikisha wananchi wa hapa mnapata huduma za afya badala ya kwenda kwenye kata nyengine”Alisema

 

MWisho.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments