NEC KUWACHUKULIA HATUA WASIMAMIZI WATAKAOHARIBU UCHAGUZI


Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema itawachukulia hatua za kisheria wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo na kata watakaoharibu uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, hivyo imewataka wasimamie sheria na taratibu za uchaguzi, ili kuepuka kuiingiza nchi kwenye machafuko.

Mkurugenzi wa tume hiyo Dkt.Wilson Mahera ametoa onyo hilo mjini Songea alipozungumza na wasimamizi wa uchaguzi kutoka mikoa ya Ruvuma, Njombe, Iringa, Lindi na Mtwara kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi, ili uchaguzi ufanyike kwa amani.

Dkt.Mahera amesema vituo vya kupigia kura vimeongezeka kilinganishwa na vile vya mwaka 2015.

Wakati huo huo Kamishna wa tume hiyo Jaji Mstaafu Thomas Mihayo mewahadharisha waratabu na wasimamizi wa uchaguzi kuwa watalazimika kufidia gharama za uchaguzi wa marudio endapo watasababisha matokeo yatenguliwe na mahakama.

Aametoa hadhari hiyo jijini Mwanza alipozungumza na waratibu na wasimamizi wa uchaguzi kutoka mikoa mbalimbali.

Wasimamizi na waratibu hao wa uchaguzi wamekutana na tume hiyo ili kukumbushana masuala muhimu ya kufanikisha uchaguzi mkuu.

Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amewasisitiza wazingatie maelekezo ya ujenzi wa vituo vya kupigia kura.

Pia Tume hiyo ya Uchaguzi NEC imesema taasisi tisini na saba za hapa nchini na kumi na saba za nje zimekidhi vigezo vya kuwa waangalizi kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments