CHADEMA YATAKA MCHAKATO WA KUANDAA MAWAKALA UANZE MAPEMA ILI WAAPISHWE | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, October 18, 2020

CHADEMA YATAKA MCHAKATO WA KUANDAA MAWAKALA UANZE MAPEMA ILI WAAPISHWE

  Malunde       Sunday, October 18, 2020

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewataka wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge kupitia chama hicho, washirikiane na viongozi wa chama kuanza mapema mchakato wa kuandaa mawakala wao, ili waapishwe na wasimamizi wa uchaguzi, kama sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi inavyoelekeza.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho Mhe.Tundu Lissu ametoa agizo hilo alipokuwa akiomba kura kupitia mikutano yake katika majimbo na Bahi na Kongwa mkoani Dodoma.

Mhe.Lissu ambaye amekamilisha kampeni zake katika majimbo matano ya mikoa ya Singida na Dodoma ameendelea kuwaomba Watanzania wampigie kura nyingi za ndiyo zitakazompa ushindi utakaomwezesha kuunda serikali itakayoongozwa na CHADEMA


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post