MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM, DR MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA KISIWA CHA ZANZIBAR LEO

Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amesema kuwa uchaguzi utakaofanyika Oktoba 28, ni uchaguzi wa kufanya uamuzi juu ya hatima ya Muungano wa Tanzania pamoja na tunu za Taifa.

Akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Mnazi Mmoja visiwani Zanzibar, Magufuli amesema kuwa kuna baadhi ya viongozi wamekuwa wakionesha nia ya kuvunja muungano huo, na hivyo amewataka wananchi kuwa makini kwani kura watakazopiga ndizo zitakazotoa uamuzi.

Amewataka wananchi kumchagua yeye kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt. Hussein Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar ili waendelee kuzilinda tunu za nchi ikiwemo muungano.

“Uchaguzi huu ni muhimu sana, ni uchaguzi wa kuamua, ama tuendelee na muungano wetu, ama tusiendelee nao. Ni uchaguzi wa kuamua kuwachagua viongozi wanaojua mahitaji ya sasa ya Zanzibar, ama kuwachagua watu wenye uchu wa madaraka.

“Uchaguzi huu ni uamuzi wa kuchagua watu wenye nia ya kuteteaa masilahi ya Taifa ikiwemo kutetea wananchi wanyonge na maliasili za Taifa letu ama kuchagua vibaraka ambao wanawania uongozi kwa ajili ya kutetea masilahi ya watu wengine,” amesema Dkt. Magufuli.

 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments