KAMATI YA MAADILI YA UCHAGUZI YA TAIFA YATENGUA ADHABU YA JAMES MBATIA NA ANTHONY KOMU KUFUNGIWA KUFANYA KAMPENI KWA SIKU 7

Kamati ya Maadili ya Taifa imesitisha adhabu ya kufungiwa Wagombea Ubunge wa NCCR Mageuzi, James Mbatia (Vunjo) na Anthony Komu (Moshi V) na kuwaruhusu kuendelea na kampeni. 

Walifungiwa kufanya kampeni (17-23 Oct) kwa kutumia vipeperushi visivyoidhinishwa na Msimamizi wa Uchaguzi

Uamuzi huo umetolewa jana  Oktoba 20,2020 baada wajumbe 13 kati ya 17 walioshiriki kikao cha kusikiliza rufaa za wagombea hao kupiga kura na kuafiki kutenguliwa kwa adhabu hizo zilizotolewa Oktoba 17, 2020.

Kikao cha kamati ya maadili jimbo la Vunjo kilimtia hatiani Mbatia kwa kutumia kipeperushi ambacho hakijaidhinishwa na msimamizi na Komu akapatikana na hatia ya kutumia bango ambalo halikuidhinishwa.

Wagombea hao wakapewa adhabu ya kutofanya kampeni kwa siku saba kuanzia Oktoba 17 hadi Oktoba 23, 2020 lakini hawakuridhika na adhabu hizo wakaamua kukata rufaa kamati ya maadili ya taifa.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments