IGP Sirro Awaonya Wanasiasa Kuacha Kuwatumia Vibaya Vijana


 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewaonya baadhi ya wanasiasa nchini kuacha kuwatumia vibaya wananchi hususan vijana hasa katika kipindi hiki cha kampeni za kuelekea kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 2020 na kuwaingiza kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani.

IGP Sirro amesema hayo akiwa Musoma mkoani Mara kwenye kikao kilichowahusisha viongozi wa kisiasa wakiwemo wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu waliopo mkoani humo ambapo aliwataka wagombea hao kutumia majukwaa ya kampeni kuhubiri amani.

Kwa upande wake mgombea ubunge jimbo la Bunda kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Ester Bulaya, amesema katika kipindi hiki cha wiki mbili kilichobaki kuelekea uchaguzi mkuu lazima vyama vishikamane na kuwa makini sambamba na kulipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments