CRDB YAJIPANGA KUTATUA CHANGAMOTO KWA WAKULIMA WA MAZAO YA KIMKAKATI

 

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa akikata keki na wateja wa benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ambayo huadhimishwa ifikapo mwezi Oktoba kila mwaka .
Baadhi ya wateja wa Benki ya CRDB tawi a Mbuyuni wakiwa wamejumuika na wafanyakazi wa Benki hiyo katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ambayo huadhimishwa mwezi Oktoba kila mwaka   
Meneja wa Benki ya CRDB kanda ya kaskazini Chiku Issa akigonga "Cheers" na mteja wa Benki hiyo Dkt Shangali wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja .
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiongozwa na Meneja wa Benki ya CRDB kanda ya Kaskazini Chiku Issa (mwenye miwani) wakiandaa chapai kwa ajili ya wateja wa benki hiyo tawi la Mbuyuni-Moshi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Meneja wa Benki ya CRDB kanda ya Kaskazini ,Chiku Issa akiandaa Chapati kwa ajili ya wateja wa benki hiyo tawi la Mbuyuni mjini Moshi .
Chapati zilizoandaliwa na wafanyakazi wa Benki ya CRDB -tawi la Mbuyuni mjini Moshi wakikata vipande vipande ili kugawa kwa wateja waliofika katika tawi hilo.

Na Dixon Busagaga -Kilimanjaro 

CHANGAMOTO za wizi wa fedha ,utapeli na dhuluma zilizokuwa zikiwakabili wakulima wa mazao ya kimkakati huenda sasa zitafika kikomo baada ya Benki ya CRDB kupata ufumbuzi wa changamoto hizo kwa kuanzisha akaunti maalumu ya Fahari Kilimi maalumu kwa wakulima.

Wakati dunia ikiwa katika wiki ya huduma kwa wateja iliyobeba kauli mbiu ya “Dream Team” Mashirika ya umma ,ya binafsi pamoja na taasisi mbalimbali za fedha nchini zimeungana katika maadhimisho ya wiki hii huku CRDB wakiweka wazi namna ambavyo wamejipanga kumsaidia mkulima.

Meneja wa Benki ya CRDB kanda ya Kaskazini Chiku Issa amesema wakulima katika maeneo mbalimbali wamekuwa wakipokea fedha zao kwa njia ya pesa taslimu .

“Hili limetokea zaidi maeneo ambayo yana mazao ya kimkakati kama Pamba ,Kahawa,Tumbaku,Chai na Katani ,wengi wa wakulima hawa walikuwa wanapokea kwa njia ya Cash”alisema Chiku .

“Kulikuwa na ubadhilifu mkubwa watu walikuwa hawapewi fedha zao sahihi laikini pia ilikua ni hatari sana wengi wao walikuwa wanapoteza fedha kwa matapeli lakini pia kwa kuibiwa” aliongeza Chiku.

Amesema CRDB imekuja na bidhaa nyingi tofauti  ambazo zinagusa jamii kwa kila kada ambapo akaunti ya kilimo ni maalumu kwa wakulima na kwamba haina makato ya aina yeyote na itasaidia kuendeleza kilimo.

Chiku amesema CRDB itaendelea kuboresha huduma zake ili kila mtanzania na kila mteja wa CRDB ziweze kumgusa na kuweza  kupata mikopo kwa urahisi ili kuboresha maisha yao na kwenda na uchumi wa kati.

“Benki inaungana na taasisi nyingine duniani kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kuwahudumia na kuwahamasiha kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na benki hii ili kuboresha maisha yao.”alisema Chiku.

Wiki ya huduma kwa wateja huadhimishwa kila mwaka ifikapo mwezi Oktoba ambapo taasisi,mashirika na kampuni mbalimbali huadhimisha kwa kurejesha kwa jamii sehemu ya faida iliyopatikana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments