‘BWEGE’ ATUA KWENYE MKUTANO WA MAJALIWA......ASHANGILIA NA KUUKUBALI MUZIKI WA CCM | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, October 22, 2020

‘BWEGE’ ATUA KWENYE MKUTANO WA MAJALIWA......ASHANGILIA NA KUUKUBALI MUZIKI WA CCM

  Malunde       Thursday, October 22, 2020


 MGOMBEA UBUNGE wa jimbo la Kilwa Kusini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Bw. Selemani Bungara maarufu kwa jina la Bwege ameukubali muziki wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kushangilia hotuba zake.


Bw. Bungara ambaye katika kipindi kilichopita alikuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Wananchi (CUF), amehudhuria mkutano wa kumuombea kura mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM wa jimbo hilo uliofanyika leo (Alhamisi, Oktoba 22, 2020) kwenye uwanja wa Ukote, Kilwa Kivinje, wilayani Kilwa, mkoani Lindi.

Mbunge huyo aliyemaliza muda wake katika jimbo hilo, alionekana akirekodi kwa kutumia simu yake huku akishangilia hotuba ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa wakati alipomuombea kura mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Wabunge na Madiwani wa CCM

Akizungumza na wakazi hao, Mheshimiwa Majaliwa aliwataka wakazi wa Kilwa wamchague mbunge ambaye atakuwa tayari kupitisha bajeti na kuwaletea maendeleo.

“Tanzania inahitaji watu makini na pale Bungeni siyo mahali pa vichekesho. Bunge linahitaji watu wa kuwasemea wananchi na siyo kuleta burudani wakati wengine wako kazini,” amesema.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post