WANAMUZIKI WATAKIWA KUHAMASISHA AMANI WAKATI WA KUPIGA KURA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, October 18, 2020

WANAMUZIKI WATAKIWA KUHAMASISHA AMANI WAKATI WA KUPIGA KURA

  Malunde       Sunday, October 18, 2020

 

Rais mpya wa Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO) Erick Kisanga.

Na Dotto Mwaibale

WANAMUZIKI nchini wametakiwa kuhamasisha amani katika uchaguzi mkuu na kwenda kupiga kura ifikapo Oktoba 28 ili kuwachagua viongozi wanao wataka. 

Ombi hilo limetolewa na Rais mpya wa Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO) Erick Kisanga wakati akizungunza na waandishi wa habari jijini Arusha.

"Ninawahimiza wanamuziki wote hapa nchini wajitokeze kupiga kura kwa Rais, wabunge pamoja na madiwani katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwezi huu", alisema.

Kisanga amewaomba watanzania kuombea uchaguzi huo ili Mungu atujalie kuwapata viongozi watakaoliongoza vema Taifa letu la Tanzania na kuwaomba wanamuziki kuendelea kutunga na kuimba nyimbo za kuhamasisha amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

"Wanamuziki ni watu muhimu kupeleka ujumbe haraka kwa wananchi  kupitia nyimbo zao hivyo niwaombe katika hizi siku chache zilizosalia wahamasishe kujitokeza kupiga kura na kulinda amani ya nchi. 

Kisanga alisema kila mwanamuziki mwenye sifa ya kupiga kura ajitokeze na kadi yake ya kupigia kura katika kituo alichojiandikisha ili kutimiza haki yake ya msingi na ya kikatiba.

Aidha Kisanga alilisitiza umuhimi wa kila mtanzania kuzingatia misingi ya amani na utulivu wakati mchakato huo ukiendelea, ikiwemo kufika mapema kituoni kupiga kura na kuondoka kuelekea kwenye majukumu mengine kwa mujibu wa sheria za uchaguzi ili kuepusha madhara au viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyoweza kujitokeza.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post