GULAM AFUNGA RASMI KAMPENI ZA UCHAGUZI... AJINADI KUBADILISHA MAISHA YA WANANCHI MJINI SHINYANGA

 

Mgombea udiwani Kata ya mjini manispaa ya Shinyanga (CCM), Gulam Hafeez Mukadam, akinadi sera kwa wananchi wa Kata hiyo wakati akifunga rasmi kampeni za uchaguzi 

Na Marco Maduhu -Shinyanga. 
Mgombea udiwani Kata ya Mjini manispaa ya Shinyanga kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Gulam Hafeez Mukadam, ameahidi wananchi wa Kata hiyo, kuwa endapo wakimchagua kuwa diwani wao siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu, atabadili maisha yao na kukua kiuchumi.

Mukadam amebainisha hayo leo Jumatatu Oktoba 25,2020 wakati akifunga Rasmi kampeni zake za kunadi Sera kwa wananchi wa Kata hiyo, mkutano uliofanyika kwenye mtaa wa Buzuka, ambao ulihudhuliwa pia na makada wa CCM. 

Amesema wakati akifanya kampeni za nyumba kwa nyumba kuomba kura, alikumbana na changamoto ya wananchi kutokuwa vizuri kiuchumi, hali iliyomfanya kuguswa nayo, na kuahidi kuwainua kiuchumi wananchi wote wa Kata hiyo ya Mjini. 

“Siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu, mkanipigie kura nyingi za ushindi, ili niwe diwani wenu kwa awamu nyingine tena, ambapo nimeahidi kuwainua wananchi wote wa Kata ya Mjini kiuchumi, kupitia mikopo ya halmashauri asilimia 10, Nne kwa akinamama, na vijana, na asilimia Mbili kwa walemavu,”amesema Mukadam. 

“Mnachopaswa kufanya kwa sasa ni kuunda vikundi, kuandaa katiba yenu pamoja na kufungua akaunti benki, ambapo mimi nitasimamia zoezi zima la kupata mikopo hiyo ambayo haina riba, na mtafanya shughuli mbalimbali pamoja na kufungua viwanda vidogo na hatimaye kuinuka kiuchumi,”ameongeza. 

Pia amesema ataendelea kuwaletea maendeleo wananchi kama alivyofanya kwenye awamu iliyopita, na kuibadilisha Shinyanga kuwa Jiji, ambapo Kata hiyo ya mjini ndio kitovu cha mkoa wa Shinyanga. 

Naye Mgombea udiwani wa viti maalum Manispaa ya Shinyanga (CCM) kupitia Kata hiyo ya mjini Ester Makune, amewataka wananchi siku ya uchaguzi wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura, na kuwapigia wagombea wote wa (CCM) ambao ndiyo watawaletea maendeleo. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mgombea udiwani Kata ya Mjini manispaa ya Shinyanga (CCM), Gulam Hafeez Mukadam, akinadi sera kwa wananchi wa Kata hiyo wakati akifunga rasmi kampeni za uchaguzi. Picha na Marco Maduhu
Mgombea udiwani Kata ya mjini manispaa ya Shinyanga (CCM), Gulam Hafeez Mukadam akiomba kura kwa wananchi
Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa meza kuu
Viongozi wa CCM wakiwa meza kuu
Mgombea udiwani wa viti maalum manispaa ya Shinyanga kupitia Kata ya Mjini Ester Makune akiomba kura kwa wananchi wa Kata hiyo siku ya uchaguzi wakawapigie kura wagombea wote wa CCM.
Mgombea udiwani Kata ya mjini manispaa ya Shinyanga (CCM),Gulam Mukadam, (kulia) akiwa na Mgombea udiwani wa viti maalum Ester Makune wakiomba kura kwa wananchi
Aliyekuwa mtia nia wa kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Shinyanga mjini Abdulmaliki Ibrahim, (kulia), akimnadi kwa wananchi Mgombea udiwani Kata ya mjini manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam, ili wamchague kuwa diwani wao siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28,2020.
Aliyekuwa Mtia nia wa kugombea nafasi ua ubunge jimboa la Shinyanga mjini Jimotoli Jilala, akizungumza kwenye mkutano huo wa kufunga Kampeni.
Aliyekuwa Mtia nia wa kugombea nafasi ya udiwani Kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Salum Kitumbo, akizungumza kwenye mkutano huo wa kufunga Kampeni.
Makada wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa kufunga Kampeni.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kufunga kampeni.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano wa kufunga Kampeni ukiendelea.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post