Picha : KAMPUNI YA AKO GROUP LTD YATOA MSAADA WA MIFUKO 200 YA SARUJI KUSAIDIA UJENZI MADARASA SHULE YA BUGARAMA

Kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Ako Group Limited, Athanas Kahigi akimkabidhi mifuko ya saruji Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Cosmas Magigi kwa ajili ya ujenzi wa madaras katika shule ya Msingi Bugarama.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kampuni ya Ako Group Limited inayotoa huduma ya chakula na usafi wa mazingira katika Mgodi wa Bulyanhulu imetoa msaada wa mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni 4.2 ili kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule ya Msingi Bugarama iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga.



Mifuko hiyo ya saruji imekabidhiwa Jumatano Septemba 30,2020 na Meneja wa Kampuni ya Ako Group Limited, Athanas Kahigi kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Cosmas Magigi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ambayo imefanyika katika shule ya Msingi Bugarama.



Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na wafanyabiashara wanaoshirikiana na Kampuni ya Ako Group Limited Kahigi alisema wao kama wafanyabiashara wanaofanya kazi na Mgodi wa Bulyanhulu ni sehemu ya jamii hivyo wanao wajibu kusaidia jamii inayozunguka mgodi huo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria Mpya ya Madini.


“Tulitembelea shule hii ya Bugarama na kujionea jinsi wanafunzi wanavyosoma katika mazingira yasiyo rafiki kutokana upungufu wa madarasa na wingi wa wanafunzi nasi Ako Group Ltd tukaahidi kuchangia mifuko ya saruji 200 yenye thamani ya shilingi milioni 4.2 na leo tumekuja kuikabidhi ili ujenzi wa madarasa”,alisema Kahigi.

Aidha aliwashukuru wafanyabiashara wanaoshirikiana na Ako Group Limited kuchangia vifaa vya ujenzi na fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule hiyo huku akiwataka wajiandae kuzalisha zaidi kwani mgodi utaanza rasmi kufanya shughuli za uzalishaji rasmi hivi karibuni.

Katika hatua nyingine Ako Group Ltd inaendelea kusaidia jamii kwa kufanya shughuli mbalimbali kama vile kujenga chumba cha darasa katika shule ya sekondari Bulyanhulu pamoja na kutoa ajira katika mgodi wa Bulyanhulu ambapo wameajiri wafanyakazi 69 katika shughuli za upishi,usafi wa vyumba,ofisi na udhibiti wa taka kati yao wanawake ni 30,wanaume 39 kutoka vijiji 14 jirani na mgodi.

"Katika kutekeleza sheria Mpya ya Madini kupitia kitengo cha huduma za jamii inayozunguka eneo la Mgodi wa Bulyanhulu, Ako Group Ltd imeajiri mtu mwenye ulemavu wa ngozi 'mtu mwenye ualbino' Gaspal William kutoka kijiji cha Ilogi katika kitengo cha usafi wa ofisi na tayari kikundi kipya cha wanawake cha Mkombozi kutoka Igudija tumekipa utaratibu wa usambazaji matunda safi na mbogamboga kutoka kwenye mashamba yao",aliongeza Kahigi.

Akipokea mifuko hiyo ya saruji, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala, Cosmas Magigi ambaye ni Afisa Elimu Shule za Msingi halmashauri hiyo,aliipongeza Kampeni ya Ako Group Limited ambao ni wakandarasi wazawa kusaidia sekta ya elimu ambapo baada ya ujenzi wa madarasa kukamilika watoto watasoma katika mazingira mazuri.

“Tunawashukuru sana Ako Group Ltd na wadau wengine waliojitokeza kuchangia vifaa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hali ambayo itapunguza msongamano wa wanafunzi darasani. Tunaomba wadau wengine waendelee kutusaidia ili elimu iweze kupanda katika halmashauri yetu”,alisema Magigi.

Meneja Mahusiano ya Jamii mgodi wa Bulyanhulu, Dk. Zumbi Musiba alisema mgodi huo utaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutatua changamoto zinazoikabili jamii kwani mgodi ni sehemu ya jamii hivyo lazima uwajibike kwa wananchi.

Kwa Mujibu wa Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Bugarama Kubebeka Leonard alisema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 2324, walimu waliopo ni 23,kuna upungufu wa walimu 27, madarasa yaliyopo ni 18 na kuna upungufu wa madarasa 32.

Naye Katibu wa Chama cha Ushirika Igaka, Emmanuel Kasala ambao ni miongoni mwa wadau wanaofanya biashara na Kampuni ya Ako Group Ltd waliochangia mifuko mitano ya saruji wamesema wataendelea kushirikiana na jamii kutatua changamoto zilizopo.

 Mwenyekiti wa Kijiji cha Bugarama Emmanuel Masanja Mhoja mbali na kuipongeza Kampuni ya Ako Group Ltd kwa msaada huo wa vifaa vya ujenzi pia aliuongeza Mgodi wa Bulyanhulu kupitia kitendo cha Mahusiano ya Jamii kwani kimekuwa kikishirikiana na jamii katika masuala mbalimbali kuwaletea maendeleo wananchi wanaozunguka mgodi.

Katika hafla hiyo, Kampuni ya Ako Group Ltd imetoa zawadi ya ya vyeti kwa wafanyabiashara wanaofanya kazi na Kampuni hiyo ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao,ambao ni Afrimar, Alpher Choice, Igaka, Nyakabale, Mamuu Chicken, Bufaso,Mkombozi na Juago Food Products ambapo pia walichangia vifaa vya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Bugarama kuunga mkono juhudi za Kampuni ya Ako Group Ltd.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Ako Group Limited, Athanas Kahigi akimkabidhi mifuko ya saruji Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Cosmas Magigi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya Msingi Bugarama Septemba 30,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Kampuni ya Ako Group Limited, Athanas Kahigi ,Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Cosmas Magigi na viongozi wa shule na kijiji cha Bugarama wakipiga picha ya pamoja wakati wa makabidhiano ya mifuko ya saruji.
Muonekano wa sehemu ya mifuko 200 ya saruji iliyotolewa na Kampuni ya Ako Group Limited
Trekta la Ako Group Limited likiwa limebeba mifuko ya saruji.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Cosmas Magigi (kushoto) akipokea mifuko mitano ya saruji kutoka kwa viongozi wa Chama Cha Ushirika Igaka wanaofanya kazi na Kampuni ya Ako Group Limited.
Meneja wa Kampuni ya Ako Group Limited, Athanas Kahigi akielezea kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Kampuni hiyo katika Mgodi wa Bulyanhulu ikiwa ni pamoja na kusaidia jamii inayozunguka mgodi huo. Alisema wamekabidhi mifuko 200 ya saruji ili kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule ya Msingi Bugarama. Kushoto ni Mwalimu Mkuu shule ya msingi Bugarama, Kubebeka Leonard. Wa kwanza kulia ni Meneja Mahusiano ya Jamii mgodi wa Bulyanhulu, Dk. Zumbi Musiba.
Meneja wa Kampuni ya Ako Group Limited, Athanas Kahigi akizungumza wakati wa kukabidhi mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Bugarama iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Cosmas Magigi akiishukuru Kampuni ya Ako Group Limited kuchangia mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya Msingi Bugarama.
Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Bugarama akiishukuru Kampuni ya Ako Group Limited na wadau wengine kuchangia vifaa vya ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya Msingi Bugarama.
Meneja Mahusiano ya Jamii mgodi wa Bulyanhulu, Dk. Zumbi Musiba akizungumza wakati Kampuni ya Ako Group Limited inayotoa huduma ya chakula na usafi wa mazingira katika mgodi wa Bulyanhulu ikitoa msaada wa mifuko ya saruji kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Bugarama iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Afisa Mtendaji kata ya Bugarama Prisca Joseph akizungumza wakati Kampuni ya Ako Group Limited ikitoa msaada wa mifuko ya saruji kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Bugarama iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Bugarama Emmanuel Masanja Mhoja akizungumza wakati Kampuni ya Ako Group Limited ikitoa msaada wa mifuko ya saruji kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Bugarama iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Wafanyabiashara wanaofanya kazi na Kampuni ya Ako Group Limited wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya ujenzi wa madarasa katika shule ya Msingi Bugarama.
Wafanyabiashara wanaofanya kazi na Kampuni ya Ako Group Limited wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya ujenzi wa madarasa katika shule ya Msingi Bugarama.
Wafanyabiashara wanaofanya kazi na Kampuni ya Ako Group Limited wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya ujenzi wa madarasa katika shule ya Msingi Bugarama.
Kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Cosmas Magigi akikabidhi cheti kwa mfanyabiashara anayefanya kazi na Kampuni ya Ako Group Limited.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Cosmas Magigi akikabidhi cheti kwa wafanyabiashara wanaofanya kazi na Kampuni ya Ako Group Limited
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Cosmas Magigi akikabidhi cheti kwa mfanyabiashara anayefanya kazi na Kampuni ya Ako Group Limited
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Cosmas Magigi akikabidhi cheti kwa mfanyabiashara anayefanya kazi na Kampuni ya Ako Group Limited
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala Cosmas Magigi akikabidhi cheti kwa mfanyabiashara anayefanya kazi na Kampuni ya Ako Group Limited.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527