YANGA YAZINDUA RASMI JEZI MPYA

Klabu ya Yanga leo, imezindua rasmi jezi zake mpya kwa ajili ya kuzitumia katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/2021, mbapo za Kijani zitatumika ugenini na njano nyumbani.

Jezi hizo zimeanza kuuzwa leo, kwa Tshs 35,000 katika Makao makuu ya Klabu hiyo kwenye Duka maalumu la Klabu na Maduka ya Wadhamini wao, GSM.

Katika uzinduzi huo ambapo Mjumbe wa kamati utendaji Yanga ambaye pia ni mkurugenzi wa uwekezaji GSM, Eng Hersi Said ndiye aliyezindua huku wanachama pamoja na mashabiki wa klabu hiyo wakishuhudia tukio hilo.

Mara baada ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba ambao ni wadhamini wakuu wa klabu ya Yanga, amewataka mashabiki wa timu hiyo kununua jezi halisi ili kuiongezea pato klabu hiyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post