WANANCHI BUSEGA WANUFAIKA NA MIRADI YA MAJI SAFI KWA ASILIMIA 42.7


Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera

MKUU Wilaya ya Busega, Mhe. Bi. Tano Mwera amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano kwa kuwezesha upatikanaji wa maji safi na kwa Wananchi kutoka asilimia 39 mwaka 2018 hadi asilimia 42.7 mwaka huu wa 2020.

Mhe. Tano Mwera amesema hayo katika taarifa yake ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika Wilaya hiyo ambapo amewataka Wananchi kutembea kifua mbele na kufurahia matunda ya Serikali yao chini ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

"Busega kazi zinaendelea. Utekelezaji wa kishindo wa Serikali yetu ya awamu ya tano unaonekana katika miradi ya miundombinu ikiwemo ya Maji safi.

Katika kipindi cha miaka mitano Serikali ya awamu wa Tano imefanya mambo mengi nchini na katika Wilaya yetu ya Busega." Alisema Mhe. Tano Mwera.

Ambapo alisema Serikali ya awamu ya Tano yaliyotokana na utekelezaji wa ilani ya CCM, Wilayani Busega kwa Kipindi cha Mwaka 2015 - 2020, imeendelea kuboresha miundo mbinu ya Maji kwa kuchimba Visima virefu na Vifupi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Busega.

"Wilaya imeweza kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji na kusaidia kupandisha kiwango cha upatikanaji maji toka asilimia 39 mwaka 2018 hadi asilimia 42.7 mwaka 2020." Alisema.

Aidha, aliongeza kuwa, Kwa sasa jumla ya watu 16,696 wanapata maji safi na salama kupitia vituo 311 vya kuchotea maji vinavyofanya kazi.

"Mafanikio katika sekta ya maji yametokana na utekelezaji wa miradi ya maji bomba iliyojengwa na inayoendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali.

Kuna Mradi wa maji Lamadi umekamilika na unatumika wenye thamani ya Tsh.12.8 Billion.

Mradi wa Maji Kiloleli utakaogharimu Tsh.1.4 Billion, uko hatua za mwisho  na mwishoni mwa mwezi wa huu wa Septemba maji yanaanza kutoka." Alisema. Mhe. Tano Mwera.

Pia aliitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na: 

Mradi wa Maji Lukungu umekamilika na unatumika wenye thamani ya Tsh.1.3 Billioni, Mradi wa Maji Nyashimo utakaogharimu tsh. 1.8 Billion, uko hatua za mwisho maji yataanza kutoka mwanzoni wa mwezi wa Oktoba.

Mradi wa Maji Manala Kata ya Badugu umekamilika na unatumika wenye Tsh.721 milioni. 
Mradi wa Maji Bushigwamhala Kata ya Kalemela umekamilika na unatumika unaogharimu tsh.180 Milioni.

Pia upo Mradi wa Maji Busami umegharimu tshs 300,000,000. Umekamilika na Unatumika, Mradi wa Maji Mwamigongwa umegharimu tshs 300,000,000. Umekamilika na Unatumika

Katika hatua nyingine, Mhe. Tano Mwera amewataka Wananchi w Busega na Watanzania kwa ujumla kuendelea kukihamini Chama Cha Mapinduzi CCM  na kukipigia kura nyingi za Urais, Ubunge na Udiwani ilikuendelea kuleta maendeleo zaidi.

"Oktoba 28, mwaka huu kila Mtanzania atoke kifua mbele kuhakikisha tunapiga kura nyingi za Urais kwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli. Lakini pia kuhakikisha kura nyingi kwa Wabunge na Madiwani wetu wote. Kwa Busega tunataka asilimia zote za kura ilikuvunja rekodi ya Busega ya Kijani" alimalizia Mhe. Tano Mwera.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post