UCHAGUZI WA MAREKANI: WADUKUZI WA MTANDAO WA URUSI, CHINA NA IRAN WALENGA TAARIFA ZA TRUMP NA BIDEN | MALUNDE 1 BLOG

Friday, September 11, 2020

UCHAGUZI WA MAREKANI: WADUKUZI WA MTANDAO WA URUSI, CHINA NA IRAN WALENGA TAARIFA ZA TRUMP NA BIDEN

  Malunde       Friday, September 11, 2020

Wadukuzi kutoka Urusi, China na Iran wanajaribu kuingilia Uchaguzi wa urais nchini Marekani utakaofanyika tarehe tatu mwezi Novemba kwa mujibu wa kampuni ya teknolojia ya Microsoft.

Kulingana na Microsoft, wadukuzi hao walilenga wafanyakazi pamoja na mashirika yanayoendesha kampeni za rais Donald Trump na mpinzani wake Joe Biden katika mashambulizi ya hivi karibuni.

Microsoft inasema ilifanikiwa kusitisha mashambulizi kutoka kundi la wadukuzi la Stronium la Urusi, Zirconium la China Phosphorus la Iran yaliolenga akaunti za watu binafsi na mashirika yanayohusika na kampeni ya rais Trump na mpinzani wake Biden.

Haya yanajiri wakati, idara ya usalama wa nchi, Marekani, ikiituhumu Urusi kwa kujaribu kuondoa imani ya wapiga kuru katika mfumo wa uchaguzi wa Marekani wakati huu nchi hiyo ikielekea uchaguzi wa mwzei Novemba

Mwezi Agosti, kituo cha ujasusi na usalama wa kitaifa ulisema kuwa Urusi inafanya kazi dhidi ya mgombea wa urais Joe Biden, huku ikimpendelea rais Trump kama ilivyofanya katika uchaguzi wa 2016.

Credit: RFI


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post