RAIS MAGUFULI AAGIZA POLISI KUMUACHIA MKUU WA SHULE ILIYOUNGUA MOTO KAGERA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, September 16, 2020

RAIS MAGUFULI AAGIZA POLISI KUMUACHIA MKUU WA SHULE ILIYOUNGUA MOTO KAGERA

  Malunde       Wednesday, September 16, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli ameliagiza Jeshi la polisi mkoani Kagera kumuachia huru Mkuu wa Shule ya Islamic Byamungu, anayeshikiliwa baada ya wafunzi 10 kufariki dunia na 7 kujeruhiwa kwa moto ulioteketeza bweni la wavulana.

Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo leo Septemba 16, 2020 akiwa Kagera katika mwendelezo wa kampeni zake za urais.

“Nafahamu Mkuu wa Shule iliyoungua Kyerwa ameshikiliwa na Polisi, ningeomba polisi wakati uchunguzi unaendelea mkuu wa shule wamuachie ili wadhibiti na kujua kama ilikuwa ni ajali kweli au palikuwa na uzembe,hata akiwa nje atashirikiana na Polisi, ” amesema Rais Magufuli.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post