Marekani yamuwewekea vikwazo mwendesha mashtaka wa ICC Fatou Bensouda

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo alitangaza jana kuwa Marekani imeweka vikwazo dhidi ya mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC Fatou Bensouda kwasababu ya ofisi yake kuendelea na uchunguzi wa watu wa Marekani. 

Pompeo alisema aliyeongezwa pia katika orodha ya vikwazo ni Phakiso Mochochoko mkuu wa idara ya sheria ya ICC, anayehusika na ushirikiano na hisani, kwa kutoa msaada kwa Bensouda za taarifa mbali mbali. 

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Marekani ameiita mahakama hiyo ya uhalifu wa kivita, ambayo Marekani haihusiki nayo, kuwa ni taasisi iliyovurugika na yenye ufisadi wa hali ya juu. 

Mwezi Juni , rais wa Marekani Donald Trump alitoa amri ya rais inayoweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya maafisa wa ICC wanaohusika katika uchunguzi wa vikosi vya jeshi la Marekani kwa uwezekano wa uhalifu wa kivita nchini Afghanistan.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments