Tanzia : JAJI MSTAAFU MARK BOMANI AFARIKI DUNIA

 Jaji Mstaafu Mark Bomani ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Tanzania amefariki dunia usiku wa kuamkia leo September 11, 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.


Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole ameandika kupitia Twitter  “Chama Cha Mapinduzi tumepokea kwa huzuni taarifa ya kifo cha Jaji (Mst) Mark Bomani, MwanaCCM & Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Tanzania, Uongozi unatoa pole kwa familia, wafiwa & wote walioguswa na msiba huu. Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe”





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527