MGOMBEA WA URAIS WA ZANZIBAR KUPITIA ACT-WAZALENDO, MAALIM SEIF AWEKEWA PINGAMIZI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, September 11, 2020

MGOMBEA WA URAIS WA ZANZIBAR KUPITIA ACT-WAZALENDO, MAALIM SEIF AWEKEWA PINGAMIZI

  Malunde       Friday, September 11, 2020
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imeshindwa kumteua Maalim Seif Sharif Hamad kugombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha ACT-Wazalendo baada ya kuwekewa pingamizi.


Alhamisi tarehe 10 Septemba 2020, ZEC imewateua 16 kati ya 17 waliochukua fomu na kurudisha kugombea urais wa visiwa hivyo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 27 na 28 Oktoba 2020.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Thabiti Faina, amesema, Maalim Seif ameshindwa kuteuliwa kutokana na vyama viwili vya DP na Demokrasia Makini kumwekea pingamizi.

Amesema, mapingamizi ya vyama hivyo yanafanana na yanahusu ujazwaji wa fomu za Maalim Seif kutokuwa sahihi.

Mkurugenzi huyo amesema, baada ya Maalim Seif kujibu mapingamizi hayo, tume hiyo itaamua kama ni kumteua au la.

Maalim Seif ndiye mgombea pekee anayewamia kugombea nafasi hiyo mara sita kati ya wote 17 waliojitosa kumrithi Rais Ali Mohamed Shein ambaye anamaliza muda wake kwa mujibu wa Katiba.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post