MAVUNDE:MIAKA 5 YA MWANZO NILIKUWA NAJIFUNZA NIPENI TENA MITANO NIWAFANYIE MAAJABU | MALUNDE 1 BLOG

Friday, September 11, 2020

MAVUNDE:MIAKA 5 YA MWANZO NILIKUWA NAJIFUNZA NIPENI TENA MITANO NIWAFANYIE MAAJABU

  Malunde       Friday, September 11, 2020
 Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi [CCM]Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde

Na Faustine Gimu  Galafoni,Dodoma.

Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde  amewaomba wananchi kumpa kura ili aweze kuongoza tena kwa kipindi cha miaka mitano mingine kwani miaka mitano iliyokwisha alikuwa anajifunza .

Mavunde amesema hayo katika mkutano wa Kampeni uliokuwa unafanyika kata ya Ihumwa jijini Dodoma ambapo amebainisha kuwa endapo atachaguliwa kuwa kiongozi atafanya maajabu katika jimbo hilo.

“Nataka niwahakikishie DUWASA  2020/2021 wamepanga bajeti kuhakikisha maji yanasambaa  katika eneo lote la kata ya Ihumwa,miaka mitano niliyokuwa naongoza nilikuwa najifunza vile”,amesema.

Aidha,Mavunde amesema  atahakikisha wanakamilisha suala la barabara katika kata hiyo endapo atachaguliwa tena.

“Barabara Mhe.Rais aliahidi barabara tunahakikisha mkituchagua tena tunakamilisha ,pia umeme tutahakikisha unaenea maeneo yote 34 yaliyobaki”,amesema.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post