DR MAGUFULI AAHIDI KUYAENDELEZA YALE YOTE AMBAYO BABA WA TAIFA NYERERE ALITAKA KUYAFANYA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, September 6, 2020

DR MAGUFULI AAHIDI KUYAENDELEZA YALE YOTE AMBAYO BABA WA TAIFA NYERERE ALITAKA KUYAFANYA

  Malunde       Sunday, September 6, 2020

Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amesema iwapo atapata ridhaa ya kuwa Rais kwa kipindi kingine cha miaka mitano ataendeleza yale yote ambayo Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Nyerere alitaka kuyafanya.Dkt. Magufuli alisema hayo jana wakati akihutubia wananchi waliojitokeza katika eneo la Mukendo mkoani Mara ikiwa ni muda mfupi baada ya Mama Maria Nyerere kuzungumza na wananchi kwenye mkutano huo.Mgombea huyo alisema kuwa licha ya kuwa Mwalimu Nyerere ameshafariki dunia lakini roho na mapenzi yake kwa Tanzania bado yapo.“Ametuachia taifa lililo huru linalojiheshimu, lisilotishwa na mtu yeyote,” alisema Dkt Magufuli huku akiwasisitiza wananchi kusoma na kumuelewa kiongozi huyo aliyelikomboa taifa.Kiongozi huyo tayari ametekeleza mambo kadhaa yaliyokuwa yakipigiwa chapuo na Mwalimu Nyerere ikiwa ni pamoja na kuhamishia serikali Dodoma ambapo ndipo Makao Makuu ya Tanzania na kuanza ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa maji katika Mto Rufiji.Mbali na hilo, ameahidi kuendeleza Mkoa wa Mara na kujenga uwanja wa ndege ili ndege ambazo serikali inaendelea kununua ziruke moja kwa moja kutoka mkoani humo kwenda maeneo mbalimbali.Dkt. Magufuli pia amewaasa wakazi wa Mara kuacha ukabila na kuwa na umoja kwa maendeleo yao.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post