ALICHOKISEMA NANDY KUHUSU KUWA NA UJAUZITO WA BILLNASS

MSANII wa kike kwenye muziki wa BongoFleva Nandy amefunguka kuhusu  madai ya kuwa na ujauzito wa Billnass baada ya kuonekana kula udongo kwenye mtandao wa Snapchat siku kadhaa zilizopita.


Akizungumzia hilo mbele ya waandishi wa habari Nandy amesema watu wanamsema ni mjamzito kwa sababu ya ongezeko la mabadiliko yake ya mwili wake ambayo yanasababishwa na ukuaji.

"Sina ujauzito wowote...Watu wanasema mimi ni mjamzito kwa sababu ya mabadiliko ya mwili wangu ambayo yanasababisha  kukua haraka kama kunenepa, ukiangalia familia yetu wote wanamaumbo makubwa halafu ni wanene labda na mimi ndiyo nimefikia hatua ya kuwa hivyo" amesema Nandy

Billnass na Nandy tayari wameshavalishana pete ya uchumba na kinachosuburiwa kwa hamu kubwa kwa sasa ni ndoa kati yao.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527