NKULILA AZINDUA RASMI KAMPENI ZA UCHAGUZI CCM NDEMBEZI..AOMBA APEWE MITANO TENA

Mgombea udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga David Nkulila  akiwaomba wananchi wa kata hiyo wamchague tena kuwa diwani wa kata ya Ndembezi. 

Na Suzy Butondo - Shinyanga
Mgombea udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga David Nkulila  amewaomba wananchi wa kata hiyo wamchague ili aweze kuzimalizia changamoto zilizopo ikiwemo kujenga soko la Kisasa na barabara za kata hiyo.

Nkulila ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani iliyofanyika katika kata hiyo na kuhudhuriwa na wanachama wa CCM na wananchi wa kata hiyo.

"Nawaomba sana  wananchi wangu tarehe 28 mwezi wa kumi mnichague Mimi katika kuwakilisha kata, mmchague Patrobas Katambi katika kuwakilisha jimbo pia mchagueni Rais wetu John Pombe Magufuli katika kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi mzee wa kuleta maendeleo kwa nchi yetu", amesema Nkulila.

Nkulila amesema kauli mbiu yake ni kuwasaidia wanyonge na kusimamia wafanyabiashara wote waweze kutendewa haki akisaidiana na mbunge wake Katambi pamoja na Rais Magufuli.

Baadhi ya wananchi wanaoishi kata ya Ndembezi, Jenifer Mahona na Shija Masanja wamesema wanamjua Nkulila ni mchapa kazi, hivyo hawana hofu na yeye watampigia kura na wanaamini atashinda kwani kazi zake zinajiekeza, na maendeleo aliyoyafanya yanaonekana.

"Sisi hatuna shaka na mgombea wetu udiwani kwani ni mchapa kazi mzuri na akisimamia hoja ya maendeleo inatendeka na anapenda haki si mtu wa kupindisha pindisha", amesema Masanja.

Mgombea udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga David Nkulila  akiwaomba wananchi wa kata hiyo wamchague tena kuwa diwani wa kata ya Ndembezi. Picha zote na Suzy Butondo
Mgombea udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga David Nkulila  akiwaomba wananchi wa kata hiyo wamchague tena kuwa diwani wa kata ya Ndembezi. Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527