Picha : SHIRIKA LA THUBUTU AFRICA INITIATIVES LAFANYA SHEREHE BOMBA NA AKINA MAMA DIDIA ,KUJADILI AFYA YA MAMA MTOTO



Na Marco Maduhu -Shinyanga.


Shirika la Thubutu Africa Initiatives la mkoani Shinyanga, linalotekeleza mradi wa USAID Tulonge Afya katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, limefanya Sherehe Bomba na majadiliano kwa akina mama Kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, kwa ajili ya kutoa elimu ya afya ya uzazi na kuimarisha makuzi na malezi bora kwa watoto walio chini ya miezi sita.


Sherehe hiyo imefanyika leo Jumatano Septemba 16,2020 eneo la Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kukutanisha akina mama kutoka vijiji vitano vya Kata ya Didia, viongozi wa dini, wataalamu wa afya, pamoja na Balozi wa Naweza Zuena Mohamed maarufu Shilole, ambaye pia ni msanii wa kizazi kipya Bongo Fleva.

Meneja miradi kutoka Shirika la Thubutu Paschalia Mbugani, amesema Sherehe hizo ni miongoni mwa utekelezaji wa shughuli za mradi wa USAID Tulonge afya, kupitia jukwaa la Naweza unaotekelezwa na Shirika la fhi 360 kwa kushirikiana na wizara ya afya kupitia T-Marc na Thubutu Africa Initiatives.

Amesema Akina mama hao wanapewa elimu juu ya unyonyeshaji watoto, kupeleka watoto kwenye huduma za kiafya pale wanapo hisi ni wagonjwa, kuwapatia chanjo zote, kuwalaza kwenye chandarua, pamoja na kutumia njia za kisasa za afya ya uzazi kwa kuzaa watoto kwa nafasi ili kuimarisha afya zao.

“Tumekutana na akina mama hawa kutoka vijiji vitano vya Kata ya Didia kufanya Sherehe, pamoja na majadiliano juu ya kuimarisha afya zao pamoja na watoto wao wale waliochini ya miezi sita, ambapo wanapaswa kuwa kwenye uangalizi wa hali ya juu ikiwamo kuwanyonyesha maziwa ya mama tu, bila ya kuwapa kitu chochote.” amesema Mbugani.

Naye Muuguzi Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Anna William, amewataka akina mama wilayani humo, pale watakapojifungua yale maziwa ya njano wawe wana wanyonyesha watoto wao  kwa sababu yanakinga nzuri ya mwili, na mtoto hataweza kuugua maradhi, pamoja na kumnyonyesha miezi sita bila ya kumpatia hata maji.

Aidha amewataka pia akina mama wawe wananyonyesha watoto wao kila siku mara nane au 12, hali ambayo itawasaidia kufanya uzazi wa mpango bila ya kuchoma Sindano, kunywa vidonge wala kupandikiza njiti, na hatimaye kuzaa kwa kuachia nafasi angalau ndani ya miaka miwili miwili.

Kwa upande wake Mratibu wa huduma za afya ya uzazi halmashauri hiyo ya wilaya ya Shinyanga Regina Renatusi, ametaja madhara ya kuzaa bila ya kuacha nafasi, ambapo mwanamke atakuwa na uwezo wa kupoteza maisha kutokana na kizazi kuchoka ikiwa siku ya kujifungua huwa wanamwaga damu nyingi na kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza maisha.

Balozi wa Naweza Zuena Mohamed (Shilole), ametoa wito kwa akina mama wilayani humo, elimu ambayo wamepewa waizingatie pamoja na kuwa mabalozi kwa wenzao ili kuimarisha afya zao kama wazazi, pamoja na watoto wao, na kuwalea katika makuzi mema na afya bora, huku wakijiimarisha kiuchumi sababu ya kuwa na muda wa kufanya shughuli za maendeleo, na siyo muda wote ni kulea tu watoto bandika bandua.

Nao akina mama hao akiwamo Asha Hamisi, walishukuru kwa elimu hiyo ambayo itawasaidia kuimarisha afya zao pamoja na watoto, ambapo yeye alishawahi kumnyeshwa maji mtoto wake ambapo tumbo lilijaa, na kuamua kumkimbiza hospitali kupatiwa matibabu, na alikuwa hajui kuwa mtoto aliye chini ya miezi sita haruhusiwi kupewa chochote zaidi ya maziwa ya mama tu.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI.

Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiative mkoani Shinyanga Jonathan Manyama Ifunda, akizungumza kwenye sherehe hizo Bomba za akina mama Didia.

Meneja miradi kutoka Shirika la Thubutu Africa Initiative Paschalia Mbugani, akizungumza kwenye sherehe hizo Bomba za akina mama Didia.

Doris Chirambo kutoka USAID Tulonge afya, akizungumza kwenye sherehe hizo Bomba za akina mama Didia.

Mwakilishi wa USAID Tulonge afya mkoani Shinyanga Mgalula Ginai, akizungumza kwenye sherehe hizo.

Mratibu Elimu ya afya kwa Umma kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ramadhani Shabani, akitoa elimu ya afya kwa akina mama kwenye sherehe hizo.

Muuguzi mkuu kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Anna William akitoa elimu ya afya ya uzazi kwa akina mama hao.

Mratibu wa huduma za afya ya uzazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Regina Renatus, akitoa elimu kwa akina mama hao.

Balozi wa Naweza Zuena Mohamed (Shilole), akitoa elimu ya afya ya uzazi na malezi bora kwa watoto kwa akina mama hao wa Didia.

Utoaji wa elimu ukiendelea.

Utoaji wa elimu ukiendelea.

Akina mama wakisikiliza elimu ya afya ya uzazi na malezi bora kwa watoto wao.

Akina mama wakisikiliza elimu ya afya ya uzazi na malezi bora kwa watoto wao.

Akina mama wakisikiliza elimu ya afya ya uzazi na malezi bora kwa watoto wao.

Mana mama Asha Hamisi, akielezea namna alivyopata shida baada ya kunywesha maji mtoto wake, kinyume na maelekezo ya watalaam wa afya, kuwa mtoto aliyechini ya miezi sita haruhusiwi kupewa kitu chochote zaidi ya maziwa ya mama tu.

Asteria Denis, akitoa akielezea namna elimu hiyo itakavyo msaidia kumtumza mtoto wake kiafya pamoja na yeye mwenyewe kufanya uzazi wa kuachia nafasi.

Balozi wa Naweza Zuena Mohamed (Shilole) akitoa zawadi ya Khanga kwa wanawake hao.

Zoezi la utoaji zawadi ya Khanga likiendelea.

Balozi wa Naweza Zuena Mohamed ( Shilole) akitoa burudani.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kwa sherehe na utoaji wa elimu ya afya ya uzazi na malezi bora kwa watoto waliochini ya miezi sita.

Balozi wa Naweza Zuena Mohamed (Shilole), akipiga picha ya pamoja na akina mama wa Didia.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527