" MAGUFULI AMTAKA KANGI LUGOLA KULA SAMAKI ....'SERIKALI INAZO KAZI NYINGI'

MAGUFULI AMTAKA KANGI LUGOLA KULA SAMAKI ....'SERIKALI INAZO KAZI NYINGI'


Kushoto ni Mbunge wa Mwibara aliyemaliza muda wake na kulia ni Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli.
**
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemwambia aliyekuwa Mbunge wa Mwibara Mh Kangi Lugola kuwa kwa sasa aendelee kula Samaki wake vizuri na asiwe na wasiwasi kwa kuwa Serikali inazo kazi nyingi.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 4, 2020, wakati akizungumza na wananchi wa Bunda mkoani Mara, ambapo pia amewaeleza wananchi hao sababu iliyopelekea Mheshimiwa Kangi Lugola kutochaguliwa na Halmashauri Kuu ili aweze kuwania tena nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo.

"Tukasema huyu (Lugola) ni mtu mzuri namfahamu, na makazi Serikalini yapo mengi tu na yeye ametoka ametulia wala hakubabaika, Lugola kula Samaki wako vizuri enjoy CCM ipo tu", amesema Magufuli.

Magufuli ametaja pia sababu iliyopelekea Lugola kutochaguliwa tena, "Mh Lugola na mwenzake walifungana, utawapeleka wote kugombea Ubunge?, nikapiga hesabu walipofungana kura zilikuwa 173, tukahesabu nani ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya tukakuta Lugola ni Mjumbe, kwa hiyo kura 1 alijipigia, kwa hiyo moja kwa moja, tukitoa hiyo 1 yeye anaondoka".

Via EATV

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527