ANDREW CHENGE AMHAKIKISHIA USHIRIKIANO MGOMBEA UBUNGE BARIADI MBELE YA JPM


Mh. Andrew Chenge aliyekuwa mbunge wa Bariadi akimuombea kura na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea urais Dk.John Magufuli kwa kuizungumza vizuri historia ya mwaka 1995 ya kumpa fedha kwa ajili ya mama Janeth
Mh. Andrew Chenge aliyekuwa mbunge wa Bariadi akimuombea kura na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea urais Dk.John Magufuli, Mgombea Ubunge wa jimbo hilo 
Mhandisi Mkundo Andrew Mathew ambaye ni mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi akiomba kura kwa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.

……………………………………….

 Aliyekuwa mbunge wa Bariadi mkoani Simiyu Mh. Andrew Chenge amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea urais Dk. John Magufuli kwa kuizungumza vizuri historia ya mwaka 1995 ya kumpa fedha kwa ajili ya mama Janeth ambaye naye ana upendo mkubwa sana.

"Sikutegemea kama historia ungeisema vizuri mbele ya watu”,amesema Chenge.

Dk. Magufuli alielezea historia yake ya miaka mingi inayomhusu yeye na Chenge na kusema... "Chenge mimi ni kaka yangu kweli kweli wala sio uongo, nilipoingia Bungeni mwaka 1995 mke wangu alikuwa na mimba.

”Aliyenisaidia hela kwenda hospitali shilingi 200,000 alitoa Chenge, ndio maana nasema ni zamu ya Mhandisi Mkundo Andrew Mathew, Chenge kazi zipo nyingi,”amesema Dk. Magufuli wakati anamueleza Chenge na wabunge wengine waliokuwa wakiwatumia wananchi katika majimbo yaliyokuwa katika mkoa huo.

Amewashukuru wabunge waliomaliza muda wao, katika siasa akisema “Kuna miaka 10, lakini nimezungumza maeneo mengi kazi ziko nyingi", Dk. Magufuli.

Akimuombea kura mgombea ubunge wa jimbo hilo Kundo Andrew Mathew,  Mh. Andrew Chenge amesema mwaka 2005 alipogombea walifanikiwa kulikomboa jimbo hilo kutoka upinzani.”Tutahakikisha safari hii kura zinakuwa za kutosha sana, nimhakikishie kijana wetu(mgombea ubunge) mimi Andrew Chenge tutafanya kazi ya uhakika.

Mh. Andrew Chenge ameongeza kuwa Rais Dk.John Magufuli katika kipindi cha miaka mitano ameitendea haki Bariadi, ameitendea haki Simiyu na ameitendea haki Tanzania na kupita kwake kuomba kura kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 28 anatakeleza tu matakwa ya kikatiba.

Chenge amesisitiza mbele ya maelfu ya wananchi wa Bariadi na Mkoa wa Simiyu waliohudhuria mkutano wa kampeni wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.Magufuli ambaye amefika hapo kuomba kura.

”Tutatembea bega kwa bega kuhakikisha tunapata kura za kutosha, tutakwenda kata zote 31 katika jimbo letu ingawa tayari madiwani wa kata saba wamepita bila kupingwa lakini tutakwenda kutafuta kura kwa ajili yako na wagombea mbunge na madiwani,”amesema Chenge.

Ameongeza "Ingekuwa sio matakwa ya Katiba Dk. Magufuli unapaswa kuwa Rais wa miaka mingine mitano,kwani ameitendea haki Bariadi, ameitendea haki Simiyu na ameitendea haki Tanzania".

CHANZO - FULLSHANGWE BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527