BALOZI KAGASHEKI AMUOMBEA KURA WAKILI MSOMI STEPHEN BYABATO BUKOBA MJINI


Balozi Khamisi Kagasheki (kushoto) akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Bukoba mjini Wakili Stephen Byabato
Balozi Khamisi Kagasheki akihutubia wananchi wakati akimuombea Kura mgombea ubunge Wakili Byabato
**

Na Ashura Jumapili -Bukoba
Aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo hilo kipindi Cha mwaka 2005 Hadi 2010 Balozi Khamisi Kagasheki amewaomba wananchi wa Bukoba kuungana kwa pamoja kumchagua mgombea ubunge wa Bukoba mjini, Stephen Byabato kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi na kuacha historia iliyopita.

 Balozi Khamisi Kagasheki, aliyewahi kushika nafasi ya  Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii pia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ametoa rai hiyo jana wakati akimuombea kura mgombea ubunge huyo Wakili Stephen Byabato mjini Bukoba.

Alisema umefika muda muafaka wa kumpeleka bungeni Wakili Byabato kijana msomi wa sheria ili aweze kwenda kuwatetea wananchi kwa kujenga hoja madhubuti za kisheria.

Alisema wasirudie makosa yaliyofanyika mwaka 2015 kupeleka Jimbo upinzani hivyo kuchelewesha maendeleo ya Bukoba.
Wananchi waliohudhuria mkutano huo wa hadhara wa CCM

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post