Wasimamizi Wasaidizi Wa Uchaguzi Nzega Mjini Watakiwa Kuepuka Ushabiki

NA TIGANYA VINCENT
MSIMAMIZI wa Uchaguzi wa Jimbo la Nzega Mjini Philemon Magesa amewataka Wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata kuepuka ushabaki  wa aina yoyote wa kisiasa katika utekelezaji wa majukumu yao ili kutosababisha vurugu wakati zoezi la uchaguzi mkuu ujao.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua mafunzo ya Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Mkuu ujao kutoka Kata 20 za Halmashauri hiyo.

Magesa alisema  ili Wasimamizi wasaidizi wawe salama katika zoezi hilo ni vema wakazingatia Katiba , Sheria na Kanuni zinasimamia zoezi zima la uchaguzi.

Alisema hali hiyo itasaidia kuufanya uchaguzi kuwa mzuri, wenye ufanisi na hivyo kuondoa kabisa malalamiko au vurugu wakati wote wa mchakato wa uchaguzi.

Aidha Magesa aliongeza kuwa katika utekelezaji wa majukumu yao ni muhimu wakavishirikisha vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi katika masuala ambayo wanastahili kushirikishwa.

Naye Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Glays Barthy walioteuliwa na Ttume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) ambao ni wanachama wa vyama vya siasa kuhakikisha wanajitoa katika vyama vyao ili kuweza kusimamizia zoezi kwa umakini.

Aliwataka wasimamizi wasadizi hao kuwa makini na watu wa karibu nao kwa kujiepusha kutoa maoni ambayo yanaweza kusababisha uvunjifu wa sheria za uchaguzi na kanuni zake.

“Muwe makini na ma group mnayo socialize kwa kuepuka kutoa maoni ambayo nanaweza kusababisha kuonekana unashabikia upande fulani na kusababisha vurugu” alionya.

Alisema katika kipindi chote cha zoezi la uchaguzi wanapaswa kujizuia kupenda kujadiliana na makundi mbalimbali nyakati zote za shughuli za uchaguzi.

“Tunajua baadhi yenu mna kazi za vyama vya siasa …baada ya kiapo hiki mnatakiwa kujitoa kabisa kuzungumzia mambo ya vyama vyenu ili muweze kuwatendea haki hata wote…na wale wenye ushabiki wa ndani ni vema wakaauacha ili waweze kutekeza majukumu yao kwa mujibu Katiba, Sheria na kanuni zinazosimamia uchaguzi” alisisitiza.

MWISHO


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments