TOENI TAARIFA KWA WAKATI ILI SERIKALI IWEZE KUTATUA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI-MPINA

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akilakiwa wakati alipowasili wilayani Chemba kusikiliza changamoto zinazowakabili wafugaji.
Waziri Mpina akiwa katika kikao na Viongozi wa Wilaya ya Chemba na wataalam kabla ya kuanza mkutano wa kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Kidoka kusililiza changamoto za wafugaji na kuzifanyia kazi.

Wananchi wa Kijiji cha Kidoka wakulima na wafugaji wakimsikiliza Waziri Mpina hayupo katika picha baada ya kuwasilisha Changamoto zaoWaziri wa Mifugo na  Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amewataka wananchi wa Kijiji cha Kidoka wilayani Chemba Mkoani Dodoma kutoa taarifa kwa wakati zinazohusu migogoro ya wakulima na wafugaji ili Wizara yake iweze kuifanyia kazi.

Waziri Mpina aliyasema hayo alipotembelea kijiji hicho akiwa na lengo la  kusikiliza changamoto za wafugaji ili ziweze kufanyiwa kazi ambapo changamoto nyingi zilizotajwa na wafugaji hao zinahusisha wizara mbalimbali ikiwa ni Pamoja naWizara ya Nishati,Ardhi na Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Akianisha Changamoto hizo mwananchi mfugaji wa kijiji hicho Bw.Abuu Mikidadi amesema kijiji hicho kinakabiliana na changamoto ya eneo la  malisho ya mifugo,ambapo kulikuwa na eneo la wazi lilitengwa kwa ajili ya malisho lakini limevamiwa na wakulima ambapo wafugaji wakiingiza mifugo  yao wanavamiwa na kupigwa.


Alisema pia kuna changamoto ya josho la kuogeshea mifugo ya kopa moja na pembejeo za mifugo,Akijibu hoja hizo Waziri Mpina alisema Serikali ni moja na inafanya kazi kwa kushirikiana,hivyo hawezi kuyakimbia matatizo hayo na atahakikisha anafikisha ujumbe kwa Wizara nyingine.


“Tunayo kazi ya kufanya kama Serikali kuangalia namna gani changamoto hizi zinaweza kut atuliwa kama vile  kupunguza gharama za umeme kwa kuzungumza na Tanesco kuweza kushusha tariffs ili wakulima na wafugaji kijijini hapo waweze kufanyakazi bila gharama yoyote na serikali imepunguza tozo za kuogeshea mifugo naitaleta pembejeo za mifugo na kuuzwa kwa bei elekezi” Alisisitiza.

Waziri Mpina aliendelea kusema kuwa “Kuna haja ya kukaa na Waziri wa Kilimo, kuangalia huu mradi wa Umwagiliaji Chemba unaolalamikiwa na wakulima na wafugaji unawezaje kuboreshwa ili wananchi wapate faida.” Alibainisha

Mpina alishauri viongozi wa Serikali ya kijiji na Serikali ya Wilaya wakae ili waweze kupata suluhisho sambamba na hilo alisema, “ Nitaleta timu inayoshugulikia migogoro toka Wizarani kwangu pamoja na wataalam waje hapa kutafuta majawabu yasiyo na upendeleo, asidhulumiwe mtu yoyote asinyanyaswe mtuyeyote, kila mtua pate haki yake na wataleta pamependekezo Serikalini.”Alifafanua

Aliendelea kusema kuwa na hakuna mfugaji anayeruhusiwa kuingiza mifugo kwenye  mashamba ya watu wengine, na kuwataka wananchi watoe taarifa kwa wakati kwa wataalam wa kilimo na mifugo na kwa jeshi la Police.

 “Hatuwezi kuwa na mfugaji anayedharau shughuli za wengine na hakuna anayeweza kuishinda Serikali.”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilayaya Chemba Dkt. Semistatus  Mashimba alisema  kufuatia changamoto ya matumizi makubwa ya umeme wananchi waliomba serikali kwa kupitia shirika la umeme nchini TANESCO kuwaunganisha na umeme wa Solar ambapo mapendekezo hayo yanafanyiwa kazi yakienda sambamba na kuangalia uwezekano wa wananchi hao kuhamishiwa katika tariff ndogo ili waweze kumudu gharama.


Kwa upande wa kuuza mazao ya wakulima, Mkurugenzi huyo alisema serikali  hailazimishi mkulima yoyote kuuza mazao kwa mfumo wastakabadhi ghalani bali mkulima yupo huru kupeleka mazao popote anapotaka.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post