TUNDU LISSU ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS WA TANZANIA


Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema Tundu Lissu amekabidhiwa fomu za kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020 na Tume ya Taifa (NEC) jijini Dodoma.



Lissu na mgombea wake mwenza, Salum Mwalimu amekabidhiwa fomu hizo leo Jumamosi tarehe 8 Agosti 2020 na Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu, Semistocles Kaijage.

Kabla ya kukabidhi fomu hizo, Jaji Kaijage amesema, siku ya uteuzi ni tarehe 25 Agosti 2020 na siku hiyo wagombea watakuwa na fursa ya kuwasilisha fomu hizo.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Charles Mahera amesema  kuna suala la kutafuta wadhamini katika mikoa 10 kati ya hizo, mikoa miwili iwe ya Zanzibar na kila mkoa mmoja angalau uwe na wadhamini 200.






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post