NIDA YAFUNGA MITAMBO MIPYA KUMALIZA TATIZO LA VITAMBULISHO | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, August 9, 2020

NIDA YAFUNGA MITAMBO MIPYA KUMALIZA TATIZO LA VITAMBULISHO

  Malunde       Sunday, August 9, 2020
Na Samirah Yusuph

Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA imefunga mitambo miwili ya kisasa kwa ajiri ya kukamilisha uzalishaji wa  vitambulisho uliokwama.

Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa mamlaka hiyo Geofrey Tengeneza alisema, hapo awali mitambo ilichakaa na kufikia hatua ya kuzalisha vitambulisho 200 hadi 500 kwa siku hali iliyofanya kuwa na mrundikano wa vitambulisho ambavyo vinasubiri kutengenezwa.

"Katika kituo chetu kikuu cha uzalishaji mitambo ilichoka na ikawa inazalisha kwa kiwango kidogo na hiyo ilitufanya kishindwa kufikia malengo yetu ya kutoa vitambulisho kwa wakati," alisema.

Aliongeza kuwa, kwa sasa wamejipanga kumaliza tatizo hilo kwa sababu wamefunga mitambo mikubwa ambayo kwa saa moja itazalisha vitambulisho 4500. na kwa siku vitazalishwa 144,000.

"Mitambo tuliyoifunga kwa sasa tunaamini ndani ya muda mchache tutamaliza zoezi la kutoa vitambulisho, niwaombe wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi ili wapate vitbulisho na ambao tayari wana namba waende ofisi za mtaa wakachukue vitambulisho.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi kutunza vitambulisho vyao, kwani umapo poteza atakibidi kuweza kulipia kiasi cha Sh 20000 kwa ajili ya kitambulisho kingine.

"Watu wengi wanakuwa hawapo makini katika kutunza vitambulisho hivi niwatake wananchi kuvitunza kwa dhati kuepuka usumbufu pindi kipoteapo," alisema.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post