NEC YAONYA MAZOEA USIMAMIZI UCHAGUZI MKUUTume ya taifa ya uchaguzi (NEC) imewaonya wasimamizi wa uchaguzi mkuu ngazi ya majimbo kutoka mkoa wa Shinyanga na Simiyu, ambao walishasimamia zoezi la uchaguzi awamu nyingi, kutofanya kazi hiyo kimazoea katika uchaguzi wa mwaka huu, bali wazingatie sheria za uchaguzi na maelekezo ya tume.

Hayo yamebainishwa leo mjini Shinyanga na Kamishina wa Tume ya taifa ya uchaguzi Balozi Omari Mapuli, wakati akifunga mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya majimbo kutoka mkoa wa Shinyanga na Simiyu, yaliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo namna ya kusimamia zoezi zima la uchaguzi ili lifanyike huru na haki bila ya kutokea dosari zozote zile zitakazo sababisha vurugu.

Amesema katika zoezi la kuteua wasimamizi wa uchaguzi mkuu ngazi ya majimbo tume hiyo ilichagua wapya na wale ambao ni wazoefu, na kuwataka pale watakapokuwa wakitekeleza majukumu yao wazingatie maelekezo watakayopewa na tume, na siyo kufanya kazi kimazoea, ili kuepuka malalamiko na vurugu wakati wa mchakato wa uchaguzi.

“Naombeni sana wasimamizi wa uchaguzi mkuu mzingatie mafunzo ambayo mmepewa na tume ya taifa ya uchaguzi, pamoja na kufuata sheria za uchaguzi, na kutofanya kazi kimazoea ili uchaguzi ufanyike huru na haki, na kusiwepo na malalamiko yoyote yale ambayo yatasababisha vurugu na kuchafua amani ya nchi,’ amesema Mapuli.

“Kwenye changamoto kubwa ambazo hamna uwezo wa kuzitatua wasilianeni na tume ya taifa ya uchaguzi zitatuliwe, ili kuepuka kujiingiza kwenye migogoro ambayo itavuruga zoezi la uchaguzi ,” ameongeza.

Pia amewataka wasimamizi hao wa uchaguzi, watakapokuwa wakiteuwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura, wachague watu wenye uwezo mzuri wa kufanya kazi, pamoja na kuwapa kipaumbele wale ambao ni wazoefu na waliofanya vizuri kwenye chaguzi zilizopita.

Katika hatua nyingine amewataka waandae maeneo mazuri kwa ajili ya kupokea vifaa ya uchaguzi pamoja na kuimarisha ulinzi, ikiwa suala la uchaguzi ni zito sana na halihitaji kufanyiwa mzaha.

Naye mkurugenzi idara ya habari na elimu ya mpiga kura Givness Aswile kutoka tume ya taifa ya uchaguzi, amewataka wasimamizi hao wa uchaguzi mkuu ngazi ya majimbo mafunzo ambayo wamepewa wakayatoe pia kwa ufasaha kwa wasimamizi ngazi ya Kata, ili uchaguzi ufanikiwe ngazi zote na kumalizika salama.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Kamishina wa Tume ya taifa ya uchaguzi Balozi Omari Mapuli, akifunga mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya majimbo kutoka mkoa wa Shinyanga na Simiyu.

Mkurugenzi msaidizi idara ya utawala na rasilimali watu Clement Berege kutoka tume ya taifa ya uchaguzi, akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo na kuwasisitiza wasimamizi hao wa uchaguzi mkuu wazingatie sheria za uchaguzi.

Mkurugenzi idara ya habari na elimu ya mpiga kura Givness Aswile kutoka tume ya taifa ya uchaguzi, akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.

Msimamizi wa uchaguzi mkuu ngazi ya majimbo kutoka Simiyu James John, akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake kutoka Simiyu na Shinyanga na kuahidi kuzingatia sheria za uchaguzi na maelekezo kutoka tume ili uchaguzi ufanyike huru na haki.

Wasimamizi wa uchaguzi mkuu ngazi ya majimbo kutoka Shinyanga na Simiyu, wakiwa kwenye ufungaji wa mafunzo ya usimamizi kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Wasimamizi wa uchaguzi mkuu ngazi ya majimbo kutoka Shinyanga na Simiyu, wakiwa kwenye ufungaji wa mafunzo ya usimamizi wa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post