NEC YAMTEUA TUNDU LISSU KUWA MGOMBEA URAIS WA TANZANIA KUPITIA CHADEMA

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemteua Tundu Lisuu kuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema na mgombea mwenza, Salum Mwalimu katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020. 

Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Bara amekuwa mgombea wa 15 leo kuteuliwa na Mwenyekiti wa NEC, Semistocles Kaijage kuwania nafasi hiyo kupeperusha bendera ya Chadema kwenye uchaguzi huo unaoshirikisha vyama vingi.

Wengine walioteuliwa ni; John Pombe Magufuli (CCM), Leopard Mahona (NRA), John Shibuda (Ada Tadea), Mutamwega Mgaiwa (SAU), Cecilia Augustino Mwanga (Demokrasia Makini), Yeremia Maganja (NCCR-Mageuzi) na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF.

Pia wamo, Philip John Fumbo (DP), Bernard Membe (ACT- Wazalendo), Qeen Cuthbert Sendiga (ADC), Twalib Ibrahim Kadege (UPDP), Hashimu Rungwe (Chaumma), Khalfan Mohamed Mazurui (UMD) na Seif Maalim Seif (AAFP).

Baada ya kuhitimisha kwa uteuzi kwa wagombea hao, kutakuwa na muda wa uwekaji mapingamizi kwa mujibu wa sharia na mwisho ni kesho tarehe 26 Agosti 2020 saa 10 jioni.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527