MCHAKATO WA KUBADILI JINA LA UWANJA WA TAIFA KUWA BENJAMIN MKAPA STADIUM WAKAMILIKA | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, August 22, 2020

MCHAKATO WA KUBADILI JINA LA UWANJA WA TAIFA KUWA BENJAMIN MKAPA STADIUM WAKAMILIKA

  Malunde       Saturday, August 22, 2020
Mchakato wa kubadili jina la Uwanja wa Taifa kuwa Benjamin Mkapa Stadium (Uwanja wa Benjamin Mkapa) umekamilika.


Kubadilishwa kwa jina la uwanja huo ni moja ya njia za kumuenzi Hayati Benjamin Mkapa, aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu.

Akiwa madarakani Hayati Mzee Mkapa alipigania vyema sekta ya michezo nchini na kufanikisha kujenga Uwanja wa Taifa. 

Baada ya kifo chake yaliibuka maoni kutoka kwa watu na taasisi mbalimbali kuhusu uwezekano wa kubadili jina la uwanja huo na kwa kuwa lilikuwa wazo zuri, Rais Dkt. John Magufuli aliafiki na shughuli ya kubadili jina ikaanza mara moja.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post