JESHI LA MALI LATANGAZA KUANDAA SERIKALI YA MPITO BAADA YA KUIPINDUA SERIKALI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, August 19, 2020

JESHI LA MALI LATANGAZA KUANDAA SERIKALI YA MPITO BAADA YA KUIPINDUA SERIKALI

  Malunde       Wednesday, August 19, 2020

Vikosi nchini Mali vimemuondoa madarakani rais Ibrahim Boubacar Keïta na kutangaza azma yao ya kuunda serikali ya mpito kabla ya uchaguzi mpya.

Hii inakuja baada ya rais Keïta kuonekana kwenye televisheni akisema kuwa amejiuzulu.

Yeye na waziri mkuu walisindikishwa kwa mtutu wa bunduki kutoka mji mkuu Bamako hadi kwenye kambi ya jeshi.

Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wamepinga kuchukuliwa kwa uongozi wa nchi na jeshi la Mali.

Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za magharibi, Ecowas, lilitangaza kufunga mipaka nanchi hiyo na imesitisha uhusiano wa kifedha nanchi hiyo.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litakutana baadae Jumatano.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post