HII HAPA RATIBA YA ROBO FAINALI EUROPA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, August 7, 2020

HII HAPA RATIBA YA ROBO FAINALI EUROPA

  Malunde       Friday, August 7, 2020

Viungo matata wa Klabu ya Manchester United, Paul Pogba (Kulia) na Bruno Fernandes wakipongezaka kwa kazi nzuri.

Klabu ya Wolves imetinga hatua ya robo fainali ya mashindano ya Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya takribani miaka 48 baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya bao 2-1 dhidi ya Olimpiacos ya Ugiriki.

Bao pekee lililoivusha Wolves liliwekwa kimiani na mshambuliaji Raul Jimenez aliyefunga kwa penati dakika ya 8 ya mchezo, kufuatia jitihada za Daniel Podence kuzaa matunda baada ya kuangushwa kwenye eneo la hatari na mlinda mlango wa Olimpiacos, Bobby Allain.

Jimenez ambaye ni raia wa Mexico, alifunga bao hilo na kumfanya awe mchezaji pekee wa ligi kuu ya England aliyehusika moja kwa moja katika mabao mengi msimu wa 2019/20 wa mashindano yote, ambaye katika michezo 37,alifunga mabao 27 na pasi zilizozaa mabao 10.Kwa ushindi huo, Wolves ilisonga mbele kwa jumla ya ushindi wa bao 2-1 na sasa watachuana na itaumana na Sevilla ambayo iliiondosha AS Roma kwa jumla ya mabao 2-0.

Matokeo mengine, Bayer 04 Leverkusen iliifunga Rangers kwa bao 1-0 na kusonga kwa jumla ya bao 4-1na sasa Wajerumani hao watakipiga dhidi ya Inter Milan ya Italia ambayo iliifunga Getafe bao 2-0.

Manchester United ambayo iliifunga bao 2-1 klabu ya LASK katika mchezo wa mwisho, sasa wataumana na FC Copenhagen hatua vilabu vya Shaktar Donetsk watakipiga dhidi ya FC Basel na michezo hiyo itapigwa kuanzia August 10 na 11.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post