ACT WAZALENDO WAANZA MCHAKATO KUWAPATA WAGOMBEA URAIS, UBUNGE, MADIWANI


Chama cha ACT Wazalendo kimeanza maandalizi ya Mkutano Mkuu wa kupitisha wagombea wa ngazi mbalimbali kwa ajili ya kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba, mwaka huu.


Kamati Kuu ya ACT Wazalendo inakutana leo jijini Dar es Salaam kwenye kikao cha maandalizi ya Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 5, mwaka huu.

Chana hicho kimejidhatiti kusimamisha wagombea katika ngazi zote za urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mgombea urais wa Zanzibar, wawakilishi, wabunge na madiwani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post