WANANCHI MSALALA WATAKIWA KUTUMIA WAKANDARASI WANAOTAMBULIKA TANESCOMeneja wa Mgodi wa uchenjuaji Dhahabu wa Msalala Gold,Zameer Ahmed akitoa maelekezo juu ya mota za Umeme zenye kutumia umeme mdogo kwa watendaji wa TANESCO.
Mhandisi Mkuu idara ya uatafiti Tanesco makao makuu,Aurea Bigirwamungu mwenye T-Shirt ya Mistari na Monica Masawe kutoka Shirika hilo wakimsikiliza kwa makini Meneja wa Msalala Gold Ltd,Zameer Ahmed.
Afisa Mkuu Masoko wa TANESCO,Monica Masawe akitoa elimu ya usalama kwa wakazi wa Kijiji cha Segese,katika Halmashauri ya Msalala.
Mwananchi wa Kata ya Segese Peter ,Raphael akielezea changamoto zinazowakabili wananchi wa Kata hiyo juu ya Nishati ya Umeme.
Na Ali Lityawi - Kahama
Wananchi katika Halmashauri ya Msalala,wilaya ya Kahama,mkoani Shinyanga wametakiwa kutumia wakandarasi wanaotambulika na TANESCO,kuunganisha nishati ya umeme majumbani na viwandani ili kuepuka majanga yanayotokana na nishati hiyo.

Hayo yalisemwa na Mhandisi Mkuu Idara ya Utafiti wa Shirika la umeme Nchini (TANESCO) Aurea Bigirwamungu wakati walipokuwa katika ziara ya kikazi ya kutoa elimu kwa watumiaji wakubwa wa umeme na wa kati katika vijiji vya Segese na Kakola,vilivyo Halmashauri hiyo.

Akizungumza na wachimbaji wadogowadogo wa migodi, wamiliki wa Viwanda vidogo vidogo,Mhandisi Bigirwamungu aliwaomba wananchi wa maeneo hayo kuwa na matumizi bora ya nishati ya umeme kuepuka ajali, ikiwa sambamba na kuboresha na kulinda mali zao kwa usalama.

Alisema ajali za umeme hutokea na kuhatarisha maisha ya watu na mali zao  pindi ufungwaji wa miundombinu hiyo ikifanywa na mafundi wasio na weledi hususani wa mitaani na hivyo kuleta maafa katika jamii iliyopo katika maeneo husika.

Alisema kuwa TANESCO inatambua mafundi ambao wamesajiliwa na EWURA,na kubainisha kuwa ajali nyingi za umeme zinazosababishwa na uwepo wa mafundi wasio na leseni kufanya kazi hizo.

Aliongeza kuwa kutokana na uwepo wa mafundi hao wa mitaani imekuwa sababu kwa nyakati kadhaa kuibuka kwa ajali nyingi na pengine maafa huku kutofahamika waliohusika inakuwa rahisi kuchukuliwa hatua na kuwawajibisha.

Alisema kuwa TANESCO ipo kwa ajili ya kutoa miongozo ya utumiaji salama wa umeme na kuacha kufunga kamba za chuma kwenye makenchi pamoja na kuwatahadharisha wananchi juu ya upitishaji wa nishati chini ya ardhi na kuunganishiana kiholela kwani zinaweza kuleta maafa ya kuuwa watu pale nyaya zinapo chunika.

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa masoko kutoka Tanesco Monica Massawe alisema kuwa serikali inawekeza sana katika uzalishaji wa umeme na kuimarisha moiundombinu yake ili wateja wawe na matumizi bora ya Nishati hiyo.

Aidha aliwakumbusha kujiepusha gharama zisizo za msingi kwa kuanzisha utamaduni wa kutumia vifaa na mashine na mitambo inayotumia umeme kidogo ili kupunguza gharama za matumizi yake.

Mmoja wa Wananchi wa kata ya Segese Hosea Kajuna walilitaka shirika hilo kusambaza umeme kwa haraka kwenye maeneo ambayo tayari yana nishati hiyo ambayo hayajafikiwa na wakala wa umeme vijijini (REA) ili kuongeza idadi ya watumiaji wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post