TBC YATOA TAMKO CHADEMA KUFUKUZA WATANGAZAJI WA TBC KATIKA UFUNGUZI WA KAMPENI ZA CHADEMA

TAMKO LA TBC KUFUKUZWA KATIKA UFUNGUZI WA KAMPENI ZA CHADEMA

Dar es Salaam: Agosti 28, 2020

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake katika mkutano wao wa kuzindua Kampeni za Mgombea wao wa Urais katika viwanja vya Zakheim, Mbagala Jijini Dar es Salaam, jioni hii.


TBC1 na TBC Taifa kama chaneli za umma zilikuwa zinarusha matangazo ya moja kwa moja kwenye uzinduzi huo kwa mujibu wa sheria na miongozo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mwongozo wa Tume wa mwaka 2020, (kifungu e na j), kanuni za maadili ya tasnia ya habari; vyombo vya utangazaji vya umma pia vinao wajibu wa kuhakikisha maudhui yanayorushwa hewani yanazingatia maadili ya taaluma na ya jamii.

Kitendo cha uongozi wa CHADEMA kutangaza kuwafukuza watangazaji wa TBC si cha kiungwana na kinahatarisha usalama wa watendaji hao na vifaa vyao.

Pamoja na kwamba TBC inapanga kutoa taarifa rasmi Polisi na kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa sasa inasitisha rasmi kurusha matangazo ya CHADEMA hadi hapo watendaji wake watakapohakikishiwa usalama.

TBC inapenda kutimiza wajibu wake wa kisheria na imekuwa tayari, siku zote, kufanya kazi na vyama vyote vya siasa bila ubaguzi.


TAZAMA VIDEO HAPA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post