MAONESHO YA PICHA 'WATU WA TANZANIA' KUFANYIKA KWA SIKU MBILI KITUO CHA ALLIANCE FRANCAISE JIJINI DAR | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, August 1, 2020

MAONESHO YA PICHA 'WATU WA TANZANIA' KUFANYIKA KWA SIKU MBILI KITUO CHA ALLIANCE FRANCAISE JIJINI DAR

  Malunde       Saturday, August 1, 2020
Rania Nasser ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha Tano ameandaa maonyesho ya picha yanayojulikana kama 'Watu wa Tanzania' ambayo yatafanyika Alliance Francaise jijini Dar es Salaam tarehe 7 na 8 Agosti 2020.

Matumizi ya picha na video kuelezea stori au hadithi ni muhimu Sana, yanaelimisha, kubadilisha Habari za kuhadithiwa na muonekano pamoja na kuleta mabadiliko chanya kwa Dunia. Tumeona mfano mingi kwenye hili. Mabadiliko yanaanza kwa kubadilisha maono ya jamii.

Tangu akiwa na umri mdogo, Rania ametembelea sehemu mbali mbali za nchi yake Tanzania na sehemu zote hizo ambazo ametembelea na watu aliokutana nao, na Habari zile ambazo amezipata, ameona kilicho bora kwa Watanzania.

Rania pia ameweza kutembelea nchi zingine ulimwenguni lakini ukarimu na upole wa Watanzania umekuwa ni wa kipekee.Wakati wa kutembelea nchi hizo zingine, Rania ametengeneza marafiki wengi. Kitu kimoja ambacho ameweza kutambua ni kwamba wengi wanajua machache kuhusu Bara la Afrika, na Sana Sana Tanzania.

 Anasema 'naelewa ya kwamba kuna watu hawajui ya kwamba Afrika sio nchi, na hii sio kwa kila mtu, siwezi kupata picha kwa umasikini unaokumba vijiji vyetu, mapigano kwenye Miji yetu, magonjwa na mengine mengi'
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post