MGOMBEA URAIS TANZANIA ATAKA MAKAHABA,MASHOGA WACHAPWE VIBOKO 200

Mgombea urais  nchini Tanzania kupitia Chama Cha Kijamii (CCK), David Mwaijojele, amesema iwapo wananchi watakipa ridhaa chama chake kushika madaraka, serikali yake itatunga sheria ambayo makahaba, wasagaji na mashoga watakuwa wanachapwa viboko 200 na kwenda jela miezi sita.

"Mwili wa mtu si wa kufanyia biashara kingono, makahaba, wasagaji na mashoga wanaitia aibu nchi. Naomba wananchi wanikabidhi nchi nitawanyoosha," amesema Mwaijojele.

Amesema suala la rushwa limekuwa tatizo sugu nchini, hivyo serikali yake itahakikisha linashughulikiwa ipasavyo ili liishe kabisa.

Amesema mafisadi, watakatishaji fedha na wanaotorosha fedha nje watapewa adhabu ya kwenda jela miaka 50 na kupigwa viboko 200 baada ya kuhukumiwa.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527