TUNDU LISSU APITISHWA KWA KISHINDO CHADEMA KUGOMBEA URAIS TANZANIA

Tundu Lissu, amependekezwa na wajumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Demokarsia na Maendeleo (Chadema) kuwa mgombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.
 

Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema amesema, Lissu amepata kura 405 ya kura zote 442 za wajumbe waliopiga kura jana jioni.
 
Jumla ya wapigakura 442
1. Tundu Lissu kura 405
2. Lazaro Nyalandu kura 36
3. Dkt. Mayrose Majinge kura 1.
 
Ikiwa, mkutano mkuu huo utampitisha, Lissu anakwenda kuchuana na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Pombe Magufuli ambaye naye amekwisha kupitishwa na chama chake.

Wagombea wengine wa urais na vyama vyao kwenye mabano ni, Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Hashimu Rungwe (Chaumma) na John Shibuda wa Ade- Tadea.

Aidha,Baraza Kuu la chama hicho limependekeza kwa mkutano mkuu wa chama hicho, Salum Mwalimu kuwa mgombea mwenza wa urais wa Tanzania

Mwalimu ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar amependekezwa jana Jumatatu tarehe 3 Agosti 2020 na leo Jumanne atathibitishwa na mkutano mkuu. 

Pia Baraza Kuu la CHADEMA limempendekeza kwa Mkutano Mkuu wa chama hicho, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Zanzibar), Said Issa Mohamed kuwa mgombea Urais wa Zanzibar.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527